Vitu Nane (08) Vya Kufanya Kabla Ya Kuuza Nyumba Yako.
Sanaa na sayansi ya kuuza nyumba ni moja ya eneo muhimu sana katika uwekezaji katika ardhi na nyumba. Sanaa ya kuuza nyumba inahitaji kujulikana na kila mwekezaji. Usipofahamu sanaa ya kuuza nyumba, unahitaji wa kukusaidia kuweza kufanya hilo.
Leo nimeakuandalia makala hii kwa lengo maalumu la kukusisitiza umuhimu wa maarifa sahihi ya kuuza nyumba yako. Kuuza nyumba ni moja ya njia ya kutengeneza pesa. Hivyo unahitaji mbinu suluhishi za mazungumzo bora sana. Katika kitabu cha LUGHA YA BIASHARA YA VIWANJA NA NYUMBA nimeeleza kwa undani zaidi kuhusu mazungumzo bora yanavyoweza kukusaidia kuuza kwa bei ya juu.

Kupitia kitabu hicho unaweza kuuza kwa bei ghali na bado ukaweza kutengeneza mahusiano bora sana na wawekezaji wanunuzi. Rafiki yangu jipatie kitabu hicho kikusaidie kupiga hatua kubwa.
Huhitaji haraka sana kuweza kuuza nyumba yako. Pia huhitaji kupoteza muda kwa sababu zisizo za msingi. Andaa kila mpango wa mauzo ya nyumba yako.
Vifuatavyo ni vitu nane (08) vya kufanya kabla ya kuuza nyumba yako:
Tafuta Dalali Makini Sana.
Hakikisha unatumia dalali mwaminifu. Dalali awe anajiheshimu na ana heshimu kazi yake. Kwa hapa Tanzania ni kawaida kuwapata madadali ambao hawapendi kazi zao. Madadali wengi hawajui hata mambo ya kisheria yahusuyo uwekezaji katika ardhi na nyumba.
Na wengi wao hawatambuliki kisheria kama ni madalali wa ardhi na nyumba. Wengi wa madalali wa ardhi na nyumba hawana utaratibu maalumu wa kulipwa ada ya huduma wanayotoa.
Kagua Matatizo Yote Katika Nyumba.
Hakikisha unatumia milango ya fahamu kumvutia mnunuzi wa nyumba zako. Jicho ni mlango wa fahamu wenye nguvu sana. Anza na matatizo yanayohusiana na macho. Baada ya hapo, kagua matatizo yanahusiana harufu.
Harufu ndio kitu cha pili ninachokipa kipaumbele katika kuangalia matatizo ya nyumba yako. Katika uwekezaji katika ardhi na nyumba kuna msemo unasema " kinachonuka huwezi kuuza ". Hakikisha hakuna harufu ya aina yoyote. Usiseme harafu nzuri.
Unaweza kuona kuna harufu nzuri lakini mteja wako akaona hakuna harufu nzuri hata kidogo. Hivyo unahitaji timu yako kwa ajili ya kuhakikisha jambo hili. Hakikisha hakuna gesi hatarishi kwa afya ya binadamu.
Mlango wa tatu muhimu sana katika biashara ya ardhi na nyumba ni Masikio. Hakikisha hakuna sauti za ovyo. Sauti za ndege wa ajabu, mbwa na paka. Hakikisha unaweka vifaa vya kuzuia sauti hizo kama zipo.
Mlango wa nne wa fahamu muhimu ni ngozi. Hakikisha nyumba yako haina milima. Hakikisha ukipitisha mkono usihisi mchanga wa aina yoyote. Hakikisha uchafu wote unaoweza kugusa umetoweka kabisa.
Ukuta usiwe na misumari ambayo itakuwa hatarishi kwa wapangaji wa mwekezaji mnunuzi unayotegemea kumuuzia. Kila kitu kinachoweza kuumiza ngozi na huleta hisia mbaya kwa atakayeishi humo ndani unakishgulikia ipasavyo.
Mlango wa tano wa fahamu ni ulimi. Hapa Unahakikisha hakuna madini yenye sumu. Madini mazito kama mekyuri, radiamu, na maji ya kunywa. Maji yenye chumvi nyingi huweza kuwa kikwazo kwa mnunuzi wako.
Hakikisha una njia mbadala ya kumsaidia kupunguza chumvi katika maji ya kutumia nyumbani kwake. Unaweza kumwekea kitwamisho maji au kifaa cha kuchemshia maji kabla hayajatumika kwa matumizi ya binadamu.
Unaweza kukodi mkaguzi aliyebobea katika masuala ya biashara ya ardhi na nyumba. Au kagua mwenyewe kama huwezi kukodi mkaguzi kutoka nje ya kampuni lako.
Andaa Nyumba Yako Kuchukua Picha Ya Matangazo.
Kwa sababu kutangaza nyumba yako katika mitandao ya kijamii au mtandao wa intaneti ni jambo muhimu mno. Usipange kutofanya. Utajifunza mambo mengi. Utapata mawasiliano ya wawekezaji wengine ambao wanaweza kununua nyumba zako nyingine tofauti na nyumba ya sasa.
Mambo ya kuzingatia katika kuandaa mazingira ya kuchukua picha ni kama ifuatavyo:
Moja, usafi wa ndani na nje ya nyumba yako. Hakikisha unasafisha hasa kiasi kwamba kusiwepo na dosari lolote katika picha yako.
Vyombo vya kigitali vinachukua picha ambazo ni rahisi sana kuonyesha dosari hata ndogo sana. Hivyo jitahidi kuonyesha usafi wa kiwango cha juu sana. Itasaida kuwavutia wawekezaji makini mno. Wengi hurusha picha zenye vipande vya mbao vimezaa huko na huko.
Mara vipande vya bati na vigae. Huuuh! Ukiona tu picha mwili unasisimuka, ni kweli nyumba imejengwa vizuri lakini unajiuliza kwa nini imekuwa katika hali hiyo. Kama nyumba unajenga wewe mwenyewe hakikisha uusafi unafanyika kila siku baada ya kazi ya siku kuisha kuepuka kuchukua picha ambazo zitaharibu jina la kampuni lako.
Wataarifu Maboresho Unayotegemea Kufanya.
Hakikisha unawambia wanunuzi wako kuwa kuna huduma nyingi unaendelea kuongeza katika nyumba wanayoitaka. Andaa ramani na picha kabla na baada ya kuongeza huduma hizo.
Usidanganye, hakikisha unatimiza ahadi zako. Endapo utashindwa kutimiza ahadi omba msamaha na usirudie tena. Usisubiri ukumbushwe ndio uombe msamaha. Msamaha huongeza heshima kwa anayeomba hata kwa kuchelewa.
Hakikisha Pande Zote Za Nyumba Zinavutia Sana.
Upande wa mbele upe kipaumbele katika kuuboresha sana. Kisha upande zinazobaki. Hakikisha hakuna aina yoyote ya uchafu. Hata kama una wafanyakazi unawaamini bado unahitaji kujihakikishia kuwa kila kitu kipo sawa.
Hakikisha Umetangaza Sana.
Hakikisha umetangaza katika kurasa za Facebook. Kura nzuri ni zile zinazohusu mambo ya ujenzi, ardhi, nyumba, makazi, madalali, wawekezaji katika ardhi na nyumba na kurasa za wafanyabiashara.
Hakikisha unatangaza katika kurasa zenye " Likes " nyingi mno. Lipia kiasi kidogo kwa wamiliki wa kurasa hizo. Tangaza katika tovuti au blogu ambazo zinatoa huduma zinazohusu uwekezaji katika ardhi na nyumba. U
sitangaze katika mitandao yenye kundi la watu ambao hawafanyi chochote kuhusu maisha yao. Ni afadhali utangaze kwa watu wachache lakini ambao watakuwa makini zaidi kufuatilia huduma zako.
Fuata mwongozo hapo juu katika kutangaza Twitter, Instagram na blogu. Unaweza kutangaza mitandao mingine kama vile linkedln na Google Plus.
Andaa Mbinu Bora Ya Mazungumzo.
Mbinu bora ya mazungumzo nimeeleza sana katika kitabu changu cha LUGHA YA BIASHARA YA VIWANJA NA NYUMBA. Mbinu hizo suluhisho zitakusaidia sana kuuza kwa bei ya juu na kupunguza migogoro mingi kati yako na mwekezaji mwengine.
Unahitaji kutumia timu yako ya mazungumzo kufanikisha hilo. Mbinu za kuandaa pekee yako zinaweza zisiwe na ufanisi bora sana kuliko mbinu za kushirikiana. Mazungumzo kwa kutumia timu nimeeleza pia katika kitabu cha LUGHA YA BIASHARA YA VIWANJA NA NYUMBA. Karibu ununue kitabu hiki, kitakusaidia sana.
SOMA: VITABU VYA KISWAHILI
Tafakari Usahihi Wa Vitu Saba vya Hapo Juu.
Angalia kwa makini kutoka lile jambo la kwanza hadi la saba nililokushirikisha hapa. Angalia kama kuna ulazima wa kuongeza mambo mengine ambayo sijakushikisha katika makala hii ya leo.
Ninategemea utayatendea kazi maarifa haya makini. Haya kila la kheri.
Mwandishi Aliko Musa,
Whatsapp: 0752 413 711
majengo@mtaalamu.net,
Karibu tena