Sababu Saba(07) Za Kukufanya Umiliki Nyumba Mbili(Duplex) Za Kupangisha Eneo Moja, Na Sio Nyumba Moja(NYUMBA YA FUNGUO MOJA NA NYUMBA YA FUNGUO MBILI).
Dupleksi ni nyumba mbili zenye ukuta mmoja kati ya nyumba hizo. Dupleksi ni nyumba mbili ambazo zimejengwa kwenye kiwanja kimoja. Nyumba hizi zinaweza kuwa na paa tofauti au linalofanana kwa muonekano. Kuna faida na hasara za kumiliki nyumba za makazi za aina hii. Zinakuwa na sehemu tofauti za kuingilia, sehemu tofauti za kupikia, sehemu tofauti za kuogea na sehemu tofauti za kupumzika.
Dupleksi zinakuwa na uwanja mmoja wa michezo, bwawa la kuogelea moja, na sehemu moja ya kutengeneza vyombo vya usafiri. Huweza kuitwa NYUMBA ZA FUNGUO MBILI kwa sababu mwenye nyumba hukabidhi nyumba hizo kwa familia mbili tofauti. Lakini kwenye makala hii tutaangalia kwa undani zaidi faida saba zitakazo kufanya umiliki nyumba za aina hii:

1. Faida Za Kulipa Kodi Ya Majengo.
Unaweza kulipa kodi ndogo ya majengo kwa sababu wakati mwingine itaonekana ni nyumba moja. Kama sheria ya eneo nyumba ilipo inataja nyumba za aina hii kama nyumba moja, hapo umejiandalia nafasi nzuri ya kupata punguzo ya kodi ya majengo.
2. Dupleksi inafaa Zaidi Kwa Familia Nyingi.
Nyumba za aina hii zinafaa sana kwa familia zaidi ya moja. Ndugu mbalimbali wanaweza kukaa pamoja huku wakiendelea na maisha ya kila siku. Hujisikia furaha kukaa pamoja tena kwenye mazingira yanayofanana.
Nyumba za aina hii zinafaa kwa watu wasiojiweza waliochini ya uangalizi maalumu kama vile wajane, wagane, yatima, wazee na hata watu wenye ulemavu. Inafaa kwa uangalizi wa aina hii kwa sababu ya kiwanja kimoja chenye nyumba yenye vyumba vingi. Waangalizi wanaweza kutoa mahitaji ya msingi kwa urahisi zaidi. Wazee wanaweza kuhudumiwa kwa ukaribu na ndugu zao na jamaa wa karibu.
3. Gharama Ndogo Za Ukarabati.
Usafi wa kiwanja kimoja sio ghari kuliko viwanja viwili. Ukarabati wa nyumba mbili hizi unaweza kulipia gharama ndogo kulinganisha nyumba mbili zilizojengwa viwanja tofauti. Fundi wa kukarabati jiko, jokofu, mfumo wa umeme na maji utamlipa gharama nusu ya nyumba mbili zilijengwa viwanja tofauti au zenye kuta tofauti.
4. Kuchukua Mkopo Mkubwa Kwa Riba Ndogo.
Kama umeamua kujenga nyumba moja ya milioni ishirini kwa ajili ya kupangisha, basi jenga nyumba mbili kwenye kiwanja kimoja. Gharama za ujenzi zinakuwa kidogo, gharama ndogo za ramani ya nyumba, gharama ndogo za usimamizi wa ujenzi, gharama ndogo za kununua nyumba za aina hii, gharama ndogo za hati ya kiwanja, na gharama ndogo Za kuomba mkopo.
Utapunguza gharama kubwa kama utajenga nyumba mbili kiwanja kimoja na huku ukiwa na uwezo wa kuchukua mkopo wa kiasi kile kile cha nyumba moja. Benki wanaweza kukulipisha riba kidogo kwa sababu, mara nyingi kwao ni nyumba moja. Unajipatia kodi kubwa kwa sababu unaweza kupangisha kwa familia mbili tofauti.
SOMA: Riba Mkusanyiko Kwenye Majengo Ya Makazi
Ni rahisi kulipa mkopo kuliko nyumba moja ambayo inaweza isikaliwe na mpangaji kwa miezi kadhaa. Lakini nyumba mbili katika kiwanja kimoja zinaongeza uwezekano wa kupata wapangaji. Mpangaji wa nyumba moja kati ya hizo anaweza kumwita rafiki yake mpenzi wa familia nyingi kufuatana na huduma bora inayotoa.
5. Ujirani Wa Kuvutia.
Wapangaji wa aina moja ni rahisi kukaa katika nyumba ya aina hii. Wapangaji wa aina moja hawa wanaweza kubadilishana mawazo, watoto wao huweza kucheza pamoja, ulinzi wa mali zao kwa sababu wanaaminiana na huduma nyingine za kijamii. Nyumba za aina hii huvutia wapangaji wenye mtindo mmoja wa maisha hatimaye kuishi kama majirani.

6. Ina Faragha (Privacy) Inayojitosheleza.
Nyumba za aina hii huwafanya wapangaji wafanye mambo yao kwa faragha. Faragha ni kitu muhimu sana kwa binadamu wa kawaida. Hata kama wanaaminiana na majirani zake, bado kuna mambo yatatakiwa yawe ni siri kwao.
SOMA: Faida Tano Za Kulipa Kodi Ya Majengo
Kama nyumba moja, yenye mlango mmoja, funguo moja, jiko moja, bafu moja, gadeni moja, na eneo moja la kupaki vyombo vya usafiri. Jenga nyumba mbili zenye ukuta mkuu mmoja kwenye kiwanja kimoja ili kukamilisha faragha ya wapangaji wako.
7. Ni Njia Bora Ya Kutawanya Mtaji Fedha.
Badala ya kujenga Nyumba moja kwa milioni ishirini, jenga mbili zenye thamani ya milioni kumi kila moja. Familia moja ilisababisha moto, nyingine inaweza kuepuka na ajali hiyo. Mpangaji mmoja akipata dharura kama vile kufiwa na mume au mke, mpangaji wa familia nyingine anaweza kuwa salama. Ukikosa mpangaji nyumba moja, unaweza kupata nyumba nyingine.
Hongera kwa kujifunza mengi kupitia makala hii. Naomba usiache kunishirikisha chochote kuhusu uwekezaji katika ardhi na majengo.
Mwandishi Na Mwekezaji,
Aliko Musa.
Wasapu: 0752 413 711
alikomusa255@gmail.com, majengo@mtaalamu.net
Karibu tena!