Programu Ya Januari 2022: Njia Za Kutengeneza Fedha Kwenye Ardhi Na Majengo
Habari rafiki,
Karibu kwenye programu ya mwezi Januari kwa mwaka 2022. Programu hii itaisha tarehe 30-Januari-2022. Mwezi Februari tutakuwa na programu nyingine ya mwezi husika.
Hii ni programu maalumu kwa wanachama wa kundi la REAL ESTATE BEGINNERS.
Kundi hili ni kundi maalumu kwa ajili ya watu ambao wanajifunza kutoka chini kabisa kuhusu ardhi na majengo.
Kupitia programu hii tunaweka shabaha kujifunza kuhusu somo la aina moja tu.
Somo tunalojifunza mwezi ni NJIA ZA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE ARDHI NA MAJENGO.
Nitakushirikisha kuhusu njia hizi kulingana na mazingira yetu ya Tanzania.
Utapata nafasi ya kuchangia, kuuliza na kutoa mapendekezo kuhusu somo husika.
Kila siku tutajifunza angalau njia mbili (2) za kutengeneza fedha kwenye ardhi na majengo.
Uwekezaji Muhimu Sana Hapa Duniani.
Kuwekeza kwako mwenyewe ni njia bora sana ya kujenga mafanikio makubwa sana na yanayodumu kwa miongo (decades) mingi.
Unaweza kupata kila aina ya mafanikio makubwa lakini hayawezi kudumu kama hujawekeza kwenye kichwa chako wewe mwenyewe.
Wewe ni mali ya msingi (primary asset). Ardhi na majengo ni mali ya upili (secondary assets).
Ukitaka kufikia maono yako makubwa anza na kuwekeza kwenye akili yako wewe mwenyewe.
Na ndio maana nikakuandali programu za kila mwezi ambazo zitakusaidia wewe kujifunza juu ya kitu fulani kuhusu ardhi na majengo hatua kwa hatua.
Itakuwa rahisi kwako kuepuka makosa. Ukijifunza kwangu utapata mwanga na mbinu bora za kuanza kuwekeza kwenye ardhi na majengo na hata kukuza uwekezaji wako.
Aina Kuu Mbili (2) Za Akaunti Kwenye Uwekezaji Wa Majengo.
Kama unategemea kuwekeza kwenye majengo, ufahamu kuwa kuna akaunti mbili tu. Kama tayari umeanza kuwekeza kwenye majengo, fahamu leo kuwa kuna aina mbili tu za akaunti.
Akaunti hizi mbili ndizo hushikilia mafanikio yako makubwa unayopanga kuyafikia.
Sheria ya akaunti hizi mbili ni kwamba akaunti moja lazima iwe kiongozi wa akaunti nyenzake. Zifuatazo ni aina mbili za akaunti;-
(a) Akaunti Ya Akili Yako.
Hii ndiyo kiongozi wa aina ya pili ya akaunti. Akaunti hii hukua na kustawi pale ambapo mwekezaji kwenye ardhi na majengo hujifunza, huhudhuria semina za ardhi na majengo, husoma vitabu na huwa na kocha au menta wa kumsimamia.
Akaunti hii inapofilisika ile akaunti ya pili nayo huanza kufilisika au kuanguka kutoka juu mpaka chini kabisa.
Ndio maana wale wanaorithi fedha, wanaokota mamilioni, wanashinda michezo ya bahati nasibu na njia nyingine za kutajirika haraka huanguka muda wowote.
Unahitaji kuanza kujaza akaunti hii mapema kabisa. Masomo ya kundi la REAL ESTATE BEGINNERS yatakusaidia kujaza akaunti hii ya akili yako.
Ni rahisi sana kufanikisha maono yako ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo kama akaunti hii ina salio la kutosha.
Akaunti ya akili yako inatakiwa kuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya mabilioni ya fedha hata kabla haujapata mamilioni hayo.
Kama akili yako imeishia kubeba milioni moja, siku ukipata milioni mbili au zaidi maisha yako yataharibika.
Utaanza kutumia hovyo fedha zako ukiamini tayari umeshakuwa tajiri mpaka kufa.
Kuilisha akili yako ni jambo la lazima kama kweli unahitaji kujenga mafanikio makubwa kwenye uwekezaji huu wa ardhi na majengo.
(b) Akaunti Ya Kuhifadhi Fedha.
Hii ni ile akaunti ya kawaida ya benki, mitandao ya simu na kadhalika. Akaunti hii nayo ina mchango kuifanya akaunti namba moja iweze kustawi.
Ukiwa na fedha za kutosha kwenye akaunti hii unaweza kutenga sehemu ya fedha kwa ajili ya kukuza akili yako.
Unaweza kununua vitabu, kulipia masomo ya ardhi na majengo, kulipia ada za uanachama wa makundi ya mafunzo ya ardhi na majengo na kadhalika.
Kutumia Maarifa Na Muda Wa Wengine.
Kwenye dunia hii tunategemeana rafiki yangu. Huwezi kujenga mafanikio makubwa pekee yako. Unahitaji watu wa kukishika mkono ili kufika kule unakotaka kwenda.
Huwezi ukafahamu kila kitu, vingine utavipata kwetu ambao tumejitoa kuwawezesha wawekezaji kujenga utajiri mkubwa kupitia ardhi na majengo.
Muda ninaotumia kuandaa masomo haya, huwezi kuupata wewe. Vyanzo vya maarifa sahihi niliyonayo huwezi kuvipata wewe.
Watu ninaofahamiana nao ambao wamechangia mimi niwe hivi nilivyo huwezi kuwapata.
Elimu niliyonayo mimi haiwezi kufanana na elimu yako. Hivyo tutatofautiana jinsi ya kupata uzoefu na maarifa sahihi.
Mtandao nilionao mimi, hauwezi kufanana na mtandao wako. Hivyo ni muhimu sana kujifunza maarifa haya.
Kujitoa kwangu kuandaa na kutafuta maarifa haya sahihi kunatofautiana sana na wewe.
Hizi ni sababu ambazo zinaweza kukufanya ujiunge na huduma zangu. Huduma ninayosisitiza leo ni kujiunga na kundi la REAL ESTATE BEGINNERS.
Kwa mwezi huu januari utajifunza Njia Za Kutengeneza Fedha Kwenye Ardhi Na Nyumba. Somo hili linaweza kuwapa matokeo chanya watu wafuatao;-
✓ Watu ambao hawana viwanja wala nyumba lakini wanapenda uwekezaji huu.
✓ Watu ambao hawana mitaji fedha wanapenda kuanza kuwekeza.
✓ Watu ambao hawana mtandao wa marafiki wa kuwekeza pamoja.
✓ Watu walioanza kuwekeza kwenye ardhi na majengo lakini wamekwama na hawakui tena.
✓ Watu ambao hawana muda wa kutafuta, na kusimamia nyumba za kupangisha.
✓ Watu ambao wahitaji kujifunza vitabu vya ardhi na majengo vya lugha ya kiingereza. Lakini kwa sababu moja au nyingine imeshindikana kusoma vitabu vya kiingereza.
Lipia leo Tshs.5,000/= (Elfu Tano) ili ujifunze maarifa haya mazuri.
Muhimu; Lipia elfu tano (Tshs.5,000/=) ili kupata uchambuzi wa vitabu vya ardhi na nyumba, namna ya kuanza kuwekeza na ushauri. Kwa malipo haya utajifunza mwezi mmoja (siku 30).
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Nitumie ujumbe usemao "ARDHI NA NYUMBA CLUB" ili ujiunge BURE kwenye kundi hili la WhatsApp na Telegram.
WhatsApp; +255 752 413 711