NYUMBA 11; Kumiliki Na Kupangisha Nyumba Za Matumizi Mseto (Holding And Renting Mixed-Use Buildings)
Utangulizi
Majengo ya matumizi mseto ni aina ya majengo ambayo hujengwa katika ardhi iliyopimwa.
Ardhi hiyo inakuwa inaruhusu matumizi ya makazi na biashara, au viwanda na ofisi.
Hivyo, mwenye ardhi (landlord) anaruhusiwa kumiliki nyumba kwa ajili makazi na biashara kwa wakati mmoja.
Majengo ya aina hii yanaingiza kipato kikubwa ukilinganisha na majengo ya makazi pekee yake.
Majengo ya matumizi mseto yamegawanyika katika makundi makuu matatu (03);-
Moja, majengo ulalo ya matumizi mseto (Horizontal mixed use buildings). Haya ni majengo ambayo vyumba vya kuishi vinakuwa katika sakafu moja na vile vya biashara.
Pili, majengo wima ya matumizi mseto (vertical mixed-use buildings).
Ni aina ya majengo mseto ambayo sakafu ya chini (lower floor/Ground floor) inakuwa kwa ajili ya kutoa huduma za biashara ndogondogo.
Huduma kwa umma hutolewa katika sakafu (floor) hii.
Tatu, Nyumba za kawaida za matumizi mseto (Walkable mixed-use property). Hii inajumuisha nyumba wima na nyumba mseto ya ulalo.
Nyumba hizi (Walkable mixed-use property) zinaweza huzungukwa na ukumbi wa mikutano, na ukumbi wa soko la wafanyabishara.
Uhitaji wa nyumba za matumizi mseto umekuwa ukichangiwa na vitu vifuatavyo;-
Moja, mabadiliko makubwa katika kazi za ulimwengu wa sasa.
Pili, kukua kwa uhitaji wa apatimenti.
SOM; Njia Ishirini Na Tano (25) Za Kutengeneza Pesa Katika Ardhi Pekee.
Tatu, hisia ya ukisasa kuhusu makazi bora yenye upatikanaji wa bidhaa mbalimbali.
Nne, matumizi bora ya ardhi kwa kutengeneza miji katikati miji mikubwa.
Tano, nyumba mseto zinakuwa na ufanisi mkubwa wa kipato wakati wa anguko la uchumi kuliko nyumba za makazi au biashara pekee yake.
Faida Za Kutengeneza Pesa Kupitia Kupangisha Majengo Ya Matumizi Mseto.
Moja, kuongeza kwa mahusiano baina ya wakazi na wafanyabaishara majirani.
Pili, huifanya nyumba iwe na kipato endelevu hata wakati wa hali mbaya ya uchumi.
Tatu, wapangaji wanafurahia kuwa karibu na huduma za bidhaa mbalimbali.
Hii huwaongezea pia umaarufu na uaminifu dhidi ya wafanyabishara waliokaribu na makazi yao.
Nne, kupungua kwa gharama za ukarabati kwa muda mrefu ujao.
Hii inaweza kuonekana hasa katika majengo wima ya matumizi mseto.
Changamoto Za Kutengeneza Pesa Kupitia Kupangisha Majengo Ya Matumizi Mseto.
Moja, ugomvi kati ya wakazi na wafanyabaishara wa nyumba husika.
Hii inaweza kusababishwa hasa mipango mibovu ya ujenzi wa nyumba husika.
Hivyo kutakuwepo na kuingiliana kwa maslahi na malengo wa wapangaji hao.
Pili, wafanyabishara wanaweza kukumbana na ushindani mkubwa.
Hii inaweza kutokea pale ambapo kuna wateja wachache sana kutoka nje ya mazingira ya fremu za biashara zao.
Tatu, ni vigumu kupata mkopo kutoka taasisi za fedha ukilinganisha na majengo ya matumizi yasiyo ya mseto.
SOMA;HUDUMA YA SEMINA, USHAURI, DARASA LA WIKI, NA MAKALA
Ushauri
Huhitaji kujenga nyumba ya aina hii kama hauna mtaji fedha wa kutosha.
Mtaji fedha kutoka kujenga au kununua hadi kusimamia nyumba yako ya matumizi mseto.
Ufanisi wa mbinu ya B-R-R-R-R ni mdogo katika majengo ya aina hii ukilinganisha na nyumba za matumizi yasiyo kuwa ya mseto.
Mwandishi,
Aliko Musa.
WhatsApp: +255 752 413 711
Karibu sana.