NYUMBA 02: Kumiliki Na Kupangisha Apatimenti Kubwa Ya Makazi Ya Watu (Residential Large Apartments
Utangulizi
Apatimenti kubwa ya kupangisha ya makazi yanakuwa na pango 20 (more than 20 units).
Uwekezaji katika apatimenti kubwa ya kupangisha ni rahisi kuongeza thamani kwa kuongeza kodi, kupunguza matumizi, na kuongeza ufanisi wa kusimamia.
Uwekezaji katika ardhi na nyumba unaweza kuwa ni kipato endelevu (positive cash flow returns) kwa zaidi ya asilimia 90 kupitia apatimenti kubwa za kupangisha.
Apatimenti kubwa hujengwa katika kiwanja kimoja. Hii hupelekea kupunguza gharama za ununuzi wa ardhi.
Nyumba za aina hii zinakuwa na paa moja, geti kuu moja, na sehemu moja ya kuegesha vyombo vya moto.
Apatimenti kubwa hazifai kuwekeza kwa mbinu ya B-R-R-R-R ukilinganisha na nyumba za familia moja au mbili.
Faida Za Kutengeneza Pesa Kupitia Apatimenti Ndogo
Moja, utapata kipato kikubwa kwa mwezi ukilinganisha na nyumba za familia moja au mbili.
Pili, utaongeza uzoefu na ujuzi wa kuwekeza katika ardhi na nyumba. Hii itakusaidia sana kujiongezea maarifa kuhusu uwekezaji katika ardhi na nyumba.
Tatu, unaweza kuongeza nyumba za kupangisha kutumia kodi itokanayo na Apatimenti zako.
Nne, kutumia muda mchache kukamilisha usimamizi wa Apatimenti zako. Hii inaweza kuwa tofauti na nyumba za familia moja au mbili.
Nyumba za familia moja hutawanywa katika viwanja tofauti tofauti. Hii itapelekea utenge muda mwingi wa kusimamia nyumba zako za kupangisha za familia moja.
Changamoto Za Kutengeneza Pesa Kupitia Apatimenti Kubwa
Moja, kiasi kikubwa cha mtaji fedha. Unahitaji kiasi kikubwa ili uweze kumiliki apatimenti kubwa za kupangisha.
Pili, gharama kubwa za ukarabati. Hii ni tofauti na nyumba za kupangisha za familia moja au mbili ambazo wapangaji wanaweza kufanya baadhi ya ukarabati wao wenyewe.
Ukarabati wa majengo ya aina hii hutegemea kufanywa na mwenye nyumba karibu kila kitu.
Tatu, changamoto ya kupata wapangaji ni kubwa katika apatimenti kubwa za kupangisha (residential large apartments).
Hii ni kwa sababu nyumba za aina hii hazina mazingira ya faragha (privacy), maeneo la kutosha la kuegesha vyombo vya moto, na hazina usalama kwa wapangaji na mali zao.
Wapangaji wengi hupendelea Nyumba za familia moja au mbili ambazo zinakuwa na sifa zote zilizotajwa hapo juu.
Nne, usalama mdogo katika apatimenti kubwa za kupangisha (residential Large apartments).
Hivyo utalazimika kuhakikisha wapangaji na mali zao zipo salama.
Unaweza kuajiri mlinzi katika nyumba yako au ukamteua mpangaji mwaminifu (resident property manager).
Mpangaji ambaye atasimamia usalama wa mali zake na za wapangaji wako atalipwa kiasi kidogo cha fedha kama shukurani.
Ushauri
Endapo utatumia mbinu ya B-R-R-R-R kuwekeza katika ardhi na nyumba, chagua nyumba za kupangisha za familia moja au mbili.
Kwa kukuandikia hivyo sina maana kuwa mbinu hiyo haifanyi kazi katika apatimenti kubwa (Residential Large Apartments)
Bali ufanisi wa mbinu hiyo ni mkubwa katika nyumba za kupangisha za familia moja au mbili.
Mwandishi,
Aliko Musa.
WhatsApp: +255 752 413 711
Karibu sana.