Mlango Wa Fahamu Wenye Nguvu Zaidi Katika Mazungumzo, Wawekezaji Wengi Wanafanya Maamuzi Kutumia Huo

Rafiki mwekezaji bila shaka umewahi kusikia kuhusu milango ya fahamu. Milango ya fahamu ni viungo vikuu vitano vinavyotumika kupokea taarifa kutoka katika mazingira ya ndani ya mwanadamu au ya nje pia. Ulimi, masikio, ngozi, pua na macho ni jumla ya milango anayotumia mwanadamu kupokea taarifa.
Kuna watu ambao wanapokea na taarifa kupitia macho na kuipa nguvu hizo taarifa kuliko taarifa ambazo wamezisikia. Huamini zaidi taarifa walizozipata kwa macho kuliko taarifa walizozipata kwa kusikia. Hili ndio kundi kubwa kuliko kundi jingine, linachukua zaidi ya asilimia Sabini.

Katika uwekezaji kwenye majengo hebu chukulia watu asilimia kubwa wanaathiriwa zaidi na taarifa wanazozipokea kupitia macho. Ni vigumu sana mwekezaji ukamshawishi kuwa umejenga nyumba nzuri kupitia maandishi au simu au ujumbe wa simu. Ni lazima aone kwa macho hata kama unauzoefu wa miaka hamsini katika uwekezaji kwenye majengo.
Wapo watu wachache ambao waamini zaidi taarifa walizozipata kupitia masikio, pua(kunusa), kugusa na hata kuonja. Kuna mtu akiona tunda lipo na ubora wa hali ya juu sana hata kama limepimwa na vyombo vya kitaalamu ni lazima aonje kwanza ndio amini. Kuna mtua hata kama nyumba inaubora wa hali juu sana na iko kwenye malengo yake, lakini itamlazimu anuse kwanza kama kuna harufu mbaya au la. Kuna mtu anahisi taarifa za mazingira yake na anaamini kupitia taarifa hizo.
Soma; Mitindo Mitano Ya Mazungumzo(Negotiations)
Mwekezaji unatakiwa kujua upo kundi gani. Unataka kujua udhaifu wa kundi lako. Jua kuwa utakutana na kundi kubwa la watu wanaoamini sana taarifa walizozipata kwa macho yao kuliko ngozi, pua, ulimi, na masikio. Nyumba yako inatakiwa kuwa na harufu nzuri, tena ni vyema ukawaalika watu zaidi ya kumi ili kuamua ubora harufu ya nyumba yako. Kwenye majengo tunasema, Kama Jengo linanuka siwezi kuuza.
Nyumba yako inatakiwa kuwa na kuta laini, zisizo na milima isiyoyalazima. Mwalike mtaalamu wako ili aamue kuta yenye ubora. Nyumba inatakiwa na mfumo wa sauti mzuri. Sio kila sauti inasambaa Pango zote za nyumba kutoka kwa mtu mmoja. Nyumba yako inatakiwa iwe inavutia kwa macho, ivutie sana na yenye ubora wa hali ya juu.
Sasa kwenye mazungumzo, macho yanasehemu kubwa sana kukusaidia kufikia lengo lako. Unaposoma taarifa au pendekezo la Mwekezaji wa upande wa pili ni lazima kushangaa kwanza. Unashangaa ili kumuweka sawa na sio kuwa unamdharau au vinginevyo.
Kushangaa wakati wa kupokea taarifa mpya ni muhimu sana rafiki. Ni rahisi sana kuona kweli umeguswa kama utaonesha kwa macho. Hakuna mtu ambaye ataweza kuisoma akili yako na kuelewa nini unataka. Lakini unapotumia njia hakikisha hii hakikisha unamfahamu mwekezaji huyo kwa kiasi fulani.
Wawekezaji ambao wanaamini zaidi taarifa za kusikia ni rahisi sana kukumbuka jambo. Kama utakutana naye mahali fulani, yeye atakusahau kirahisi sana. Lakini atakumbuka karibia kila kitu mlichozungumza. Hata sauti akisikia kwa mara ya pili atakutambua hata kama hajakuona kwa macho. Hivyo rafiki mwekezaji wa aina hii unapaswa kumsomea kwanza taarifa yote kabla hujampatia.
Soma; Mbinu Ya Kuandaa Majadiliano Bora
Kama mwekezaji anatumia macho zaidi, wengi wapo kundi hili, haina haja ya kumsomea maana hata kuamini hata kidogo na atasahau karibu kila kitu. Hivyo ni muhimu sana kujua Mlango wa fahamu anaoutumia mwekezaji wa upande wa pili wa mazungumzo kuhusu uwekezaji kwenye majengo.
Kama unauza ardhi yenye vimlima visivyofaa bila shaka itakuwa ngumu kupata wateja kwa sababu ya kutokuvutia kwa macho. Kama unauza ardhi yenye harufu mbaya zaidi ya shimo la takakata au mifereji michafu ya maji, ni vigumu sana kupata wateja. Kama unauza ardhi ya aina hiyo unaweza kutopata kabisa wateja au utapata kwa ya chini sana.

Kama unauza ardhi yenye mawe ya kupita kiasi unaweza kuuza kwa bei ya ghari kwa sababu mawe hayo naweza kutumika kwa ajili ya ujenzi siku ya baadaye. Lakini kuna maeneo ambayo ardhi yenye mawe unakuwa na bei ya chini sana kwa sababu ya muonekano wa hovyo sana.
Ninatumaini tuko pamoja mpaka mwisho wa makala hii, tukutane makala ijayo kwa maarifa bora zaidi.
Mwandishi Na Mwekezaji,
Aliko Musa.
WhatsApp; 0752413711
alikomusa255@gmail.com, majengo@mtaalamu.net
Karibu tena.