Mambo Mawili Ya Kufanya Ndani Nyumba Ili Kuongeza Thamani Yake.
Mambo Mawili Ya Kufanya Ndani Nyumba Ili Kuongeza Thamani Yake.
Kuongeza thamani ni jambo muhimu sana kulifanya ikiwa kweli umeamua kutengeneza pesa katika biashara ya ardhi na nyumba. Leo tunajifunza kwa kina kuhusu kuongeza thamani ya nyumba yako kwa kurekebisha ndani ya nyumba yako tu.
Ukubwa wa chumba chako hauna uzito mkubwa, ikiwa utafahamu mbinu bora za kupamba ndani ya chumba hicho. Lakini ni vizuri kuangalia mahitaji ya mpangaji kama yanatosha kulingana na ukubwa wa chumba.
Chumba kisafi na cha kuvutia sana kinaweza kutufanya tujisikie vizuri. Kuwa na chumba kizuri na chenye ubora wa hali ya juu kinaongeza ufanisi na malengo ya mwekezaji. Yafuatayo ni mambo Mawili (02) ya kufanya ndani ya chumba ili kiwe na thamani kubwa:
Kontena Sahihi Au Vyombo Sahihi.
Mambo matatu muhimu ya kuangalia unapochagua ubora wa kontena. Mambo hayo ni kama ifuatavyo: (a) Muda wa kuharibika. Kontena inatakiwa iwe na muda mrefu wa kufikia hatua ya kuharibika kiasi kwamba kilichomo humo kiwe salama kabisa. Kwa maneno mengine, tarehe ya kuharibika ya kilimo katika kontena iwe fupi kuliko tarehe (expire date) ya kontena lenyewe. (b) Ukubwa wa kontena. Katika chumba kunatakiwa makontena amabayo yana ukubwa wa kutosha kuweza kubeba kila kitu ndani yake. (c) Mtindo wa vyombo (Style of the containers). Mtindo wa vyombo unatakiwa uwe wenye mvuto zaidi, na sio mtindo uliopitwa na wakati.
Unaweza kuchagua aina ya vyombo vya kuweka katika chumba chako. Vinaweza kuwa vyombo vya plastiki. Vinaweza kuwa vyombo vya udongo. Vinaweza kuwa vyombo vya chuma. Vinaweza kuwa vyombo vya mbao. Lakini vyombo vya mpira vinaweza kufaa zaidi kwa ajili ya mapambo. Hii ni kwa sababu kuangalia sifa tatu za hapo juu.
Jinsi Ya Kupanga Chumba.
Kufahamu namna ya kupanga chumba chako ni jambo muhimu mno. Hata kama una vyombo vya kisasa sana, kama umepanga vibaya hutapata matokeo mazuri.
Kama unataka kupangisha chumba chako, tafadhali sana sana panga vyombo vya chumba chako kwa mtindo unaofaa na wa kuvutia sana. Kama unataka kuuza chumba chako au nyumba yako hakikisha unapanga vyombo vyako kwa mtindo safi kabisa.
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati unapanga vyombo vyako ni kama ifuatavyo:
👉 Kusafisha Kabati au mavazi (Wardrobe). Hakikisha unatoa vyombo vyote ambavyo havihitaji kwa sasa na leo hii. Hata kama una vyombo ambazo utaweza kuvitumia miaka ijayo, vitenge usiweke chumba cha kupangisha na kuuza.
👉 Usining'inize Kila kitu. Sio kila kitu kinafaa kuweka juu na kikabaki kinapendeza.
👉 Pangilia nguo zako. Panga nguo zako kufuatana na rangi zake. Panga nguo zako kufuatana na msimu, matukio na urefu. Ukianza kuweka nguo ndefu upande mmoja endelea tu upande huo nguo ndefu tu. Kisha hamia kuweka nguo fupi upande mwengine . Mpaka chumba kienee ndipo uendelee na kazi nyingine ya kupamba chumba chako.
👉 Shefu. Mahali pazuri mno kwa ajili ni kutunzia begi. Lakini kwa hauna kifaa hiki au kimejaa vyombo vya aina nyingine, unaweza kutunza katika kichumba maalumu. Pia unaweza kuning'iniza katika chombo cha kuning'inizia nguo.
👉 Usisahau kuikunja vizuri vya droo iliyo katika chumba cha kuuza au kupangisha. Hii itaongeza sana mvuto wa chumba chako na pia itasaidia sana kutafuta vyombo vingine kwa uharaka zaidi.
Ninaamini umejifunza jambo la pekee sana kupitia makala hii. Karibu unishirikishe ulichojifunza.
Mwandishi Aliko Musa,
Whatsapp: 0752 413 711
majengo@mtaalamu.net
Karibu tena.