Maajabu Ya Riba Mkusanyiko Kwenye Ardhi Na Majengo Haya Hapa.
Riba mkusanyiko kwenye majengo...
Tumezoea kuona mwekezaji au mfanyabiashara anawekeza faida au kipato kwa mara nyingine. Mfano; mfanyabiashara A ana mtaji wa 100,000. Akipata faida ya 30,000, na akaamua kuongeza mtaji ukawa 120,000.
Mfanyabiashara A atakuwa anatumia faida kuzalisha faida nyingine hapo ndipo linazaliwa neno riba mkusanyiko. Kwa lugha nyingine unatumia faida ya kwanza kutengeneza faida nyingine tena na tena kwa kujirudia.
Ardhi na majengo hupanda thamani kwa njia kuu mbili (2). Nazo ni;-
✓ Mabadiliko ya soko lenyewe kutokana na uhaba wa ardhi.
✓ Uendelezaji wa ardhi/majengo ikiwemo ukarabati, kugawa ardhi, kupanda miche ya thamani, kupima viwanja, n.k.
Kwenye ardhi na majengo, kuongezeka kwa thamani huwezi kutenganisha na uwekezaji uliofanywa mwanzoni. Nina maana kuwa huwezi ikiwa kiwanja ulinunua milioni moja.
Kwa mwaka 1, kiwanja kikiongezeka thamani (au bei) kwa 10% huwezi kupata fedha itokanayo na ongezeko la 10%. Kwa namna hii ile 10% inawekezwa tena kwa kujirudia kwa lazima (inawekezwa bila matakwa yako).
Hii ndiyo maana riba mkusanyiko kwenye ardhi na majengo imekuwa ni ajabu na inakuwa inafaa sana kwa ajili ya kutunza utajiri pengine kuliko kutumia njia nyingine za kutunza utajiri.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Mbobezi wa majengo.
Bofya hapa kujiunga na kundi la mafunzo yatakayofanyika mwezi 05-Januari-2023...
https://chat.whatsapp.com/FeMEt5K2mYbKNYoPR8tRdX
Blog: www.uwekezajimajengo.wordpress.com