Kuwa Dalali Wa Ardhi Na Nyumba (Real Estate Agent).
Utangulizi.
Udalali wa nyumba, viwanja na mashamba ni moja ya njia ya kutengeneza pesa kupitia uwekezaji katika mali.
Udalali wa ardhi na nyumba unahitaji uwe makini kwa ajili ya kuhakikisha mawakala wanafanya kazi ipasavyo.
Udalali ni kiashirio kizuri sana cha kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki kampuni la uwekezaji katika mashamba, viwanja na nyumba.
Unaweza kuwa wakala na baadaye ukafungua kampuni zako za uwekezaji katika mashamba, viwanja na nyumba.
Kazi za Dalali na wakala zinaweza kutofautiana kidogo kufuatana na mahitaji ya sheria ya nchi husika.
Kwa hapa Nyumbani Tanzania, Dalali anapewa nafasi kubwa ya kushughulikia masuala ya uwekezaji katika mashamba, viwanja na nyumba kuliko wakala.
Dalali mshirika (Associate Broker) na wakala wanaweza kuwa na kazi zinafanana.
Dalali mshirika ni yule Dalali aliyechukua sifa zote za udalali na anaruhusa ya kumiliki kampuni ya udalali wa ardhi na nyumba wakati wowote anaopenda yeye.
Dalali mshirika anafanya kazi chini ya Dalali mwingine ambaye tayari ana kampuni lake kwa wakati huo.
Kazi zao hawa wawili ni kama ifuatavyo;-
Moja, kuwakilisha wanunuzi wa mashamba, viwanja na nyumba.
Pili, kuwakilisha wauzaji wa mashamba, viwanja na nyumba.
Tatu, kufanya mazungumzo ya bei ya mashamba, viwanja na nyumba.
Nne, kukamilisha malipo ya mauzo au manunuzi ya mashamba, viwanja na nyumba.
Tani, kuonyesha nyumba kwa wapangaji wageni.
Sita, kutangaza mashamba, viwanja na nyumba zinazouzwa.
Saba, kusimamia Mashamba, viwanja na nyumba.
SOMA; Pata Vitabu Vya Kiswahili
Faida Za Kuwa Dalali Wa Ardhi Na Nyumba (real estate agent).
Moja, Uhuru Wa Kufanya Kazi. Udalali unakuruhusu kupanga ratiba upendavyo wewe mwenyewe.
Unaweza kupata muda wa kufanya kazi na mawakala wengi zaidi kama utatafuta mfumo bora wa kufanya kazi.
Pili, chanzo Cha Kipato. Unahitaji juhudi tu na kiasi kidogo cha mtaji fedha.
Unahitaji bidii tu ili uweze kulipwa pesa nyingi zaidi.
Unahitaji kujenga timu yenye ufanisi mkubwa zaidi ya mawakala wako ili kutengeneza pesa zaidi na zaidi.
Tatu, Kiasi Kidogo Cha Mtaji Fedha. Huhitaji mamilioni kufungua, kuendesha na kusimamia kampuni lako la udalali.
Huhitaji pesa nyingi zaidi kwa ajili ya kutafuta viwanja, mashamba na nyumba kwa ajili ya wateja wengine.
Changamoto Za Kuwa Dalali Wa Ardhi Na Nyumba (Real estate agent).
Moja, Muda Mrefu Wa Kuanza Kutengeneza Kiasi Kikubwa Cha Pesa.
Unahitaji muda wa miaka mitatu, mitano, au hata miaka kumi ili kutengeneza mamilioni kupitia udalali wa nyumba, viwanja na mashamba.
Pili, Ni chanzo tegemezi. Kama unaumwa kipato kinaweza kupungua.
Kama utakuwa na mambo mengine yasiyohusu udalali kipato kinaweza kupungua.
Kama hutasoma vitabu, makala, magazeti yahusuyo uwekezaji katika ardhi na majengo na kupata maarifa sahihi, kipato chako kinaweza kupungua.
SOMA; Semina, Darasa La Wiki Na Makala Za Mwekezaji
Ushauri
Ni vyema zaidi kuanza kuwa Wakala wa nyumba, viwanja na mashamba na kisha unafungua kampuni la udalali.
Unaweza kuwa na kampuni la uwekezaji kwa ujumla ambalo lina idara ya udalali ndani yake.
Unapochagua kutengeneza pesa njia hii, jipe muda wa kutosha. Usitegemee upate milioni na mamilioni kwa miezi miwili au mitatu.
Unahitaji miaka ishirini au thelathini. Na uweke juhudi ya kufa au kuishi. Nina maana iwe ni kazi yako ya kudumu (Your Life Career).
Na baadaye utahitaji vibali kutoka serikalini kwa ajili ya kazi zako za udalali.
Mwandishi,
Aliko Musa.
WhatsApp: +255 752 413 711
Karibu sana.