Kuandaa Mkataba Wa Kupangisha Chumba Au Fremu Ya Biashara
Chagua mkataba wa kupangisha fremu ya biashara
Mkataba wa upangishaji unatakiwa kuwa kwenye maandishi. Epuka utaratibu wa kukubaliana na mpangaji wako kwa maneno tu.
Kwenye makala hii, ninakushirikisha mifano halisi ya mikataba tofauti tofauti ya upangishaji wa nyumba au chumba.
MFANO I; MKATABA WA KWANZA.
MKATABA WA KUPANGISHA CHUMBA CHA BIASHARA
KATI YA
BWANA ALIKO MUSA
Ambaye kwenye mkataba huu atajulikana kama mwenye nyumba halali.
NA
ADOLFU JOHN KALINGA ambaye kwenye mkataba huu atajulikana kama MPANGAJI.
MPANGAJI amekubali kupanga kwa makubaliano kama yalivyo hapa;-
(01) Kuanzia leo tarehe 22 mwezi NOVEMBA mwaka 2021 hadi tarehe 21 mwezi wa FEBRUARI mwaka 2022.
(02) MPANGAJI atalipa kodi ya pango shilingi za kitanzania 200,000 kwa maneno SHILINGI LAKI MBILI TU kwamba italipwa kwa mkupuo mmoja siku ya kuthibitisha.
(03) MPANGISHAJI akipokea fedha lazima ampe MPANGAJI stakabadhi kuonyesha amepokea malipo yote.
(04) Gharama za kodi zinaweza kubadilika wakati wowote kwa kupewa taarifa na MPANGISHAJI.
(05) Hakuna kiasi chochote cha kodi kitakachorudishwa endapo MPANGAJI ataamua kuvunja mkataba yoyote ile.
(06) MPANGAJI hataruhusiwa kupangisha nyumba kwa mtu mwingine wakati mkataba wake ni haujafikia tarehe ya mwisho bila kupata ruhusa ya mwenye nyumba.
(07) MPANGAJI atatakiwa kutunza mazingira ya nyumba pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani yake.
(08) Ukifika tarehe ya mwisho ya mkataba MPANGAJI atakabidhi chumba kwa mwenye nyumba kikiwa safi na vitu vyote vipo kama alivyokabidhiwa.
(09) Usiweke kitu chochote hatarishi bila ruhusa ya mwenye nyumba.
(10) Kama hutoendelea na mkataba mpya utamjulisha mwenye nyumba kabla ya siku KUMI (10) mkataba wako kuisha na kama utaendelea na mkataba utamjulisha mwenye nyumba pia.
Kwa kuthibitisha mkataba huu kutoka pande zote mbili, hapa chini ni sahihi ya MPANGAJI na MPANGISHAJI.
Jina kamili la MPANGISHAJI ni BWANA ALIKO MUSA.
Sahihi............... Tarehe........................
Jina kamili la MPANGAJI ni ADOLFU JOHN KALINGA.
Sahihi.................... Tarehe.....................
Anatambulika kuwa biashara yake ni Kuuza Nguo Za Kike.
MFANO II; MKATABA WA PILI.
MKATABA WA UPANGISHAJI WA FREMU YA BIASHARA.
Makubaliano haya yamefanyika siku ya tarehe 22 mwezi wa NOVEMBA mwaka 2021.
KATI YA
BWANA ALIKO MUSA wa sanduku la posta S.L.P 2998, TUKUYU-MBEYA ambaye atakuwa anatambulika ndani ya mkataba huu kama MPANGISHAJI.
NA
BIBI ENITHA P NDYUMBA wa sanduku la posta S.L.P 142, MBALIZI-MBEYA ambaye ndani ya mkataba huu anatambulika kama MPANGAJI.
Pande zote mbili wamekubaliana kama ifuatavyo;-
(a) Kwamba MPANGAJI ataendelea kuwa mmiliki halali wa chumba cha biashara kilichopo mtaa wa SIMIKE kata ya NZOVWE kilicho kwenye nyumba namba NZW/SMK0213/07.
(b) Na Kwamba MPANGISHAJI ana hiari, kwa kufuatwa makubaliano yaliyo ndani ya mkataba huu, ya kumpangisha MPANGAJI chumba cha biashara kwa ajili ya kufanyia biashara halali.
(c) Na kuwa MPANGAJI yupo tayari kwa hiari yake mwenyewe, kupanga chumba hicho kwa ajili biashara kwa kuzingatia masharti ya mkataba huu.
(d) MPANGAJI analipa shilingi 1,200,000 (SHILINGI MILIONI MOJA NA LAKI MBILI TU), malipo ambayo ni kodi ya miaka miwili kwa kiasi cha shilingi 50,000 (SHILINGI ELFU HAMSINI TU) kwa kila mwezi.
(e) Mkataba huu umeanza kutumika siku ya tarehe 25 ya mwezi wa NOVEMBA mwaka 2021 ambapo mwisho wake utakuwa ni tarehe 25 ya mwezi NOVEMBA mwaka 2023.
(f) MPANGISHAJI atatoe notisi kwa njia ya maandishi baada ya MPANGAJI kutolipa kodi zaidi ya siku 20 tangu mkataba wa awali kufikia mwisho wake.
(g) MPANGAJI anaweza kuvunja mkataba huu kwa kutoa taarifa za maandishi kwa MPANGISHAJI bila kurudishiwa kiasi chochote cha kodi iliyolipwa.
(h) Ni wajibu wa MPANGAJI kulipia bili ya umeme, maji na usafi (takataka) kwa mamlaka husika.
(i) Kwa wakati wote, MPANGAJI atatakiwa kuweka chumba katika mazingira ya usafi kwa ajili ya biashara yake.
(j) MPANGISHAJI ataomba ruhusa ya kuingia kufanya ukarabati na maboresho ya chumba kila inapohitajika.
(k) MPANGISHAJI hataruhusiwa kuongeza au kupunguza na hata kupanua sehemu yoyote bila kupata ruhusa ya MPANGISHAJI.
(l) MPANGAJI hataruhusiwa kupangisha chumba cha biashara kwa mfanyabiashara mwingine bila kupata ridhaa ya MPANGISHAJI.
(n) MPANGAJI hataruhusiwa kutumia chumba kwa hali yoyote itakayopelekea usumbufu kwa majirani zake na wafanyabishara wenzake.
(m) Na kwamba MPANGAJI anaruhusiwa kufanyia biashara halali kwenye chumba hiki kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania.
(o) MPANGAJI atakuwa huru kufanyia biashara kulingana na madhumuni yaliyo ndani ya mkataba huu bila vikwazo vyovyote.
(p) MPANGAJI atatakiwa kufanya ukarabati utokanao na uzembe au uharibifu wa makusudi wa chumba na vitu vilivyo ndani na nje ya chumba.
MPANGAJI amelipia shilingi 200,000 (LAKI MBILI TU), mbele ya mashahidi, ambayo ni kodi ya miaka miwili (sawa na miezi ishirini na nne tu).
Mkataba huu umesainiwa mbele ya;-
MPANGISHAJI
Majina kamili ni BWANA ALIKO MUSA.
Tarehe ................... Sahihi.................
MPANGAJI
Majina kamili ni BIBI ENITHA P NDYUMBA.
Tarehe................... Sahihi................
Biashara atakayofanyia ni Uuzaji wa nafaka mbalimbali.
SHAHIDI NAMBA 1
Majina kamili ni BWANA JOSEPH JAIRO MWAKASEGE
Tarehe ..................... Sahihi..............
SHAHIDI NAMBA 2
Majina kamili ni BIBI ANNA KASUKU SAATANO.
Tarehe ...................... Sahihi .................
Rafiki yangu mpendwa leo nimekushirikisha mifano miwili ya mikataba kati ya mpangaji wa fremu au chumba cha biashara na mpangishaji wa fremu au chumba cha biashara.
Muhimu; Nitumie ujumbe " Kundi La UWEKEZAJI MAJENGO" ili kupata utaratibu wa kujiunga na kundi maalumu la mafunzo ya uwekezaji katika viwanja na nyumba.
Mwandishi,
Aliko Musa
WhatsApp; +255 752 413 711
Huduma zote ninazotoa hizi hapa chini, Bofya na usome...
www.uwekezajimajengo.wordpress.com/huduma
KUJIUNGA NA KUNDI YA TELEGRAM
https://t.me/joinchat/Ydwj2U9-NKtmMGY0
Karibu sana