Jinsi Ya Kutengeneza Faida Kubwa Kwenye Kukarabati Nyumba Yako Bila Fundi Ujenzi
Weka akiba kupitia ukarabati wa nyumba yako
Utakayojifunza;-
✓ Kiasi cha faida unachotakiwa kutengeneza kwenye kukarabati nyumba.
✓ Wakati sahihi wa kumtafuta fundi ujenzi.
✓ Maswali ya kujiuliza kabla haujaamua kufanya ukarabati kwa mikono wako.
✓ Kujiandaa na dharura za ukarabati wa nyumba.
✓ Mambo matatu (03) unayotakiwa kuyapa kipaumbele.
Kiasi cha faida unayotakiwa kutengeneza
Kiasi cha kutengeneza faida kinatakiwa kupimwa kufuatana na jumla thamani ya ukarabati wenyewe. Faida haiwezi kupangwa kwa kutumia jumla ya gharama za ukarabati wa nyumba.
Fundi ujenzi anatakiwa kutengeneza faida ya asilimia 20 ya jumla ya thamani ya ukarabati wa nyumba.
Unatakiwa kutumia ripoti ya mkaguzi wa nyumba kutambua thamani ya ukarabati wa nyumba yako.
Pia, mthamini wa majengo (real estate appraiser) anaweza kukuandalia taarifa yenye kuonyesha thamani ya ukarabati wa nyumba.
Thamani hii ndiyo itakayotumika kupanga faida ya kutengeneza wakati wa kukarabati nyumba.
Hatua zote hizi zinatakiwa kufanywa na fundi ujenzi. Hii ni kwa sababu fundi ujenzi ndiye atakuwa anaifanyia ukarabati nyumba yako.
Lakini kwenye somo hili, ninakushirikisha jinsi ya kufanya ukarabati wewe mwenyewe na kuweka akiba ya faida.
Mfano, Ukarabati unagharimu jumla ya Tshs.1,000,000/= tu. Fundi ujenzi atatakiwa kupata faida si zaidi ya laki mbili (20% ya Tshs.1,000,000).
Kama utafanya mwenyewe ukarabati huu, utatakiwa kuweka akiba ya Tshs.200,000/=. Hii ni kwa sababu umekuwa fundi ujenzi wa nyumba yako mwenyewe.
Wakati Sahihi Wa Kumtafuta Fundi Ujenzi (Mtaalamu Wa Kukarabati Nyumba).
Kwa kuwa ukarabati sio lazima afanye fundi, unaweza kutumia uzoefu wako kufanya ukarabati.
Bawabu moja imeanguka, unatafuta fundi ujenzi. Bati moja linavuja, unataka kubadilisha unatafuta fundi ujenzi.
Siafu na mchwa wanajaa kwenye nyumba yako unamtafuta fundi ujenzi aje apulizie dawa.
Tofali moja au tofali tatu zimelegea unamtafuta fundi ujenzi. Koki ya maji ya bomba imekatika, unamtafuta fundi bomba.
Wewe kila kitu ni kumtafuta fundi ujenzi. Unataka kupanga samani yako kwenye nyumba, unamtafuta mtaalamu wa kupamba nyumba.
Kama ukarabati wa nyumba utakukwamisha kufanya shughuli za uzalishaji mali zaidi ya jumla ya faida itokanayo na ukarabati wa nyumba, usifanye ukarabati wewe mwenyewe.
Kama faida ni kubwa ukilinganisha na pesa utakayopata kwenye kazi zako zingine. Unahitaji kufikiria kufanya ukarabati kwa mikono yako.
Lakini ukiamua kufanya mwenyewe ni muhimu sana kuifanya kwa ubora. Na uhakikishe kweli unatengeneza faida na unaitunza faida hiyo.
Kazi hii ya kujifanyia ukarabati wa nyumba inaweza kufanyika kwenye nyumba za familia moja hadi familia nne.
Nyumba za apatimenti na majengo mengine makubwa unaweza (vyumba zaidi ya kumi). Hivyo kwenye majumba makubwa (yanayohitaji usimamizi mkubwa) ni lazima utafute fundi ujenzi wa kukarabati nyumba.
Maswali Ya Kujiuliza Kabla Ya Kufanya Ukarabati Kwa Mikono Yako.
Moja; je ninaweza kupata muda wa kusimamia mambo yote ya ukarabati wa nyumba mpaka yakamilike?
Pili; je ukiumia unaweza kutibiwa kwa bima au pesa yako mfukoni?. Hii ni kwa sababu hutakuwa na bima ya wafanyakazi eneo la kazi.
Tatu; je unayo maarifa sahihi na uzoefu wa kufanya aina ya ukarabati unaotaka kufanya?.
Nne; je unaweza kuchagua matilio bora kwa ajili ya ukarabati wa nyumba yako.
Tano; je unaweza kupata jumla ya thamani ya ukarabati wa nyumba yako?.
Haya ni maswali ambayo unatakiwa kujiuliza wewe mwenyewe kabla haujaamua kufanya ukarabati kwa mkono wako.
Kujiandaa Na Dharura Za Ukarabati Wa Nyumba.
Unapofanya ukarabati kwa mikono yako, unajiweka kwenye mazingira hatarishi. Unaweza kupata dosari fulani ambalo unaweza kupata hasara. Hatimaye ukashindwa kuweka akiba.
Lakini hii ni sio kitu ambacho unatakiwa kukiogopa. Bali unatakiwa kuongeza umakini ili uweze kupata mafanikio makubwa.
Unatakiwa na kiasi maalumu cha fedha kwa ajili ya ukarabati wa dharura. Akiba hii itasaidia sana kupunguza gharama ambazo zipo nje ya mpango wako.
Pia, unatakiwa kuwa na njia maalumu ambayo utatibiwa endapo utaumia wakati wa kufanya ukarabati wa nyumba ikiwemo bima.
Endapo muda wako una thamani kubwa ukilinganisha na thamani ya faida itokanayo na ukarabati wa nyumba unatakiwa kumuajiri fundi ujenzi wa kukarabati nyumba.
Mambo Matatu (03) Unayotakiwa Kuyapa Kipaumbele.
Moja; kuongeza thamani kwenye nyumba yako. Ukarabati wa nyumba ni njia muhimu sana kwa ajili kupandisha kiasi cha kodi.
Kama unafanya ukarabati wa nyumba kwa hovyo, hutaweza kuongeza thamani kubwa kwenye nyumba yako. Hatimaye utashindwa kupandisha kodi ya pango la nyumba yako.
Hii ni hatua muhimu sana wakati wa kukarabati nyumba. Unahitaji kuweka nguvu na akili yote kwenye ukarabati unaongeza thamani.
Achana na kuhangaika na ukarabati ambao hauongezi thamani kwenye nyumba yako. Kwa kufanya hivi, utaweza kuongeza kiasi cha kipato endelevu cha kila mwezi.
Pili; kutengeneza faida ya 20% ya jumla ya thamani ya ukarabati wa nyumba. Faida hii unatumia kuwekeza akiba. Akiba ambayo inaweza kutumika kwa ajili ya shughuli nyingine za uwekezaji kwenye majengo yako.
Tatu; kurudisha jumla ya gharama za ukarabati kupitia kodi za wapangaji ndani ya miezi ishirini au pungufu.
Hapa unachukua faida ya ukarabati jumlisha gharama ulizotumia kufanya ukarabati wa nyumba kisha unapata jumla ya gharama za ukarabati.
Hii inakuwa sahihi kama ukarabati umeufanya kwa mikono yako wewe mwenyewe. Kama utaajiri fundi ujenzi unatakiwa kuandika sifuri kwenye kipengele cha faida.
Kama utaweza kutengeneza faida ya 20% au zaidi na ukashindwa kuongeza thamani kwenye nyumba yako. Utakuwa umeshindwa moja kwa moja.
Vilevile kama utaweza kuongeza thamani kwenye nyumba yako. Lakini ukashindwa kurejesha jumla ya gharama za ukarabati ndani ya miezi ishirini na nne (24). Utakuwa umehsindwa moja kwa moja.
Mwandishi,
Aliko Musa
WhatsApp; +255 752 413 711
Huduma zote ninazotoa hizi hapa chini, Bofya na usome...
www.uwekezajimajengo.wordpress.com/huduma
KUJIUNGA NA KUNDI YA TELEGRAM
https://t.me/joinchat/Ydwj2U9-NKtmMGY0
Karibu sana