Jinsi Ya Kuanzisha Kazi Ya Kupamba Ndani Ya Nyumba Au Chumba.
Utangulizi
Kupamba nyumba ni moja ya aina ya ukarabati usio wa lazima kuufanya, lakini huongeza thamani kama ilivyo kwenye bustani ya nyumbani.
Kupamba nyumba ni moja ya njia ya kuongeza kiasi cha kodi ya pango la nyumba yako kwa sababu huongeza thamani ya nyumba unayopangisha.
Kupamba nyumba ni moja ya eneo ambalo watu hubobea ili kuingiza kipato cha kila mwezi.
Wewe pia unaweza kubobea katika eneo hili na ukajiongezea kipato maradufu.
Upambaji wa nyumba husaidia mambo yafuatayo;-
✓ Kuongeza ubora wa nyumba ya mteja wako. Anayeishi kwenye nyumba iliyopambwa huonekana bora hata katika muonekano wake kwa sababu ya ndani ya nyumba anayoishi ina mvuto.
✓ Huongeza hamasa ya kufanya kazi katika nyumba au chumba kikichopambwa.
Ukiwa na ofisi iliyopambwa utaweza kufanya kazi kwa muda mrefu kuliko kama ingekuwa unafanya kazi kwenye ofisi chafu, yenye mpangilio mbaya na harufu mbaya.
✓ Huongeza ubora wa huduma au uuzaji wa bidhaa mbalimbali. Hasa kama chumba au nyumba inatumika kwa ajili ya kufanyia biashara za huduma au biashara za huduma.
Changamoto Kutengeneza Pesa Kwa Kupamba Nyumba
✓ Hugharimu pesa. Ili kupamba nyumba yako ya kupangisha huhitaji kutoa pesa kutoka kwenye vyanzo vingine vya kipato chake.
Hivyo utahitaji kiasi cha mteja fedha ili kuweza kupamba nyumba yako. Na utahitaji kuandaa bajeti ya kupamba nyumba yako kila baada ya miezi kadhaa.
✓ Inaweza kuifanya nyumba ikose wateja au uchelewe kupata wanunuzi wa nyumba uliyopamba.
Hii hutokea sana endapo nyumba umeipamba kupitiliza na kutumia matilio ya gharama kubwa.
Jinsi Ya Kuanza Kupamba Nyumba.
Unaweza kuunganisha huduma za kupamba nyumba na huduma za kutengeneza na kupanda bustani katika nyumba za wateja wako.
Unaweza kuanza kwa kuchagua moja ya njia zifuatazo;-
(a) Kuanza bila kuwa na kampuni la kupamba nyumba.
Njia hii hufaa zaidi kwa makundi yafuatayo ya wafanyabishara;-
✓ Watu ambao wana kiasi kikubwa kidogo cha mteja fedha kwa ajili ya huduma za upambaji wa nyumba n bustani za maua kwenye nyumba.
✓ Watu ambao ndio wanaanza kazi za kupamba nyumba na hawana mtandao wa watu wenye uzoefu kwenye kazi za upambaji nyumba.
✓ Watu ambao wana muda wa kutosha kufanya kazi za upambaji nyumba wakiwemo waajiriwa katika taasisi binafsi na taasisi za umma.
✓ Watu ambao hawana uhakika juu ya ubunifu wao. Hii ni kwa sababu kazi hii huhitaji ubunifu mkubwa sana.
(b) Kuanza kwa kumiliki kampuni ya upambaji wa nyumba na bustani za maua kwenye nyumba.
Njia ya aina hii inawafaa kwa watu ambao wana sifa zifuatazo;-
✓ Watu ambao wapo tayari kusimamia waajiriwa. Kazi hii itahitaji uwe na wanatimu wabunifu na nadhifu.
✓ Mtu ambaye ana mtaji fedha kwa ajili ya kuanzisha, kusimamia na kukuza biashara ya huduma ya upambaji wa nyumba.
✓ Mtu ambaye ana maarifa na uzoefu kuhusu upambaji wa nyumba. Au mtu ambaye ameajiri mtu mwenye uzoefu na maarifa sahihi kuhusu upambaji wa nyumba.
Ushauri
Sio lazima utengeneze pesa kwa kutumia njia hii. Kuna njia nyingine nyingi za kutengeneza pesa kwenye ardhi na nyumba.
Njia nyingine ambazo unaweza kutengeneza pesa kwenye ardhi na nyumba ni kama ifuatavyo;-
✓ Kumiliki, kukarabati na kupangisha nyumba. Kupangisha nyumba ni moja ya njia ya kufikia uhuru wa kifedha kupitia ardhi na nyumba.
Wengi wa wawekezaji ambao wamefikia uhuru wa kifedha waliwekeza kiasi kikubwa cha mtaji fedha wao kwenye majengo ya kupangisha.
✓ Kununua, kukarabati na kuuza nyumba ndani ya mwaka mmoja.
✓ Kununua nyumba na kisha kuuza nyumba kwa kupangisha nyumba hiyo.
✓ Kuwekeza kwenye ardhi na nyumba kwa kuingia ubia.
✓ Kufanya kazi ya uwakala au udalali wa ardhi na nyumba. Hii ni kazi ambayo inahitaji uvumilivu na uaminifu ili kupata mafanikio makubwa sana.
Kwa miaka ya hivi karibuni, ukiwa ni dalali au wakala wa ardhi na nyumba na hutumii mitandao ya kijamii kuwafikia wateja.
Itakuwa vigumu sana kupata mafanikio makubwa kuhusu udalali wa ardhi na nyumba. Tumia nguvu ya mtandao ya kijamii kufikia mafanikio makubwa.
✓ Kufanya kazi za kuthaminisha majengo.
✓ Kununua nyumba na kuigawa katika nyumba vingi na kupangisha nyumba hiyo. Hii husaidia sana kuongeza kipato chanya kwenye nyumba yako ya kupangisha.
Pia, unahitaji kupima kipato cha kodi ya pango la nyumba kwa kila mita ya mraba moja. Pangisha nyumba kwa mita moja ya mraba.
Unaweza usimwambie mpangaji kuwa unapangisha kwa mita moja ya mraba kwa sababu mfumo huu hauzazoeleka sana kwa hapa kwetu Tanzania.
Muhimu kwenye mpango mkakati wako unahikisha unakuwa na mahesabu ya kodi ya pango la nyumba kwa mita moja ya mraba.
✓ Kuendeleza ardhi ghafi. Hapa unaweza kununua ardhi kubwa na kuigawa katika vipande vipande. Kisha vipande hivyo kwa wawekezaji kwenye ardhi.
Pia, unaweza kununua kiwanja na kujenga nyumba katika kiwanja chako kisha uza nyumba yako au pangisha.
✓ Kutoa mikopo kwa wamiliki wa viwanja au nyumba kwa ajili ya kufanyia kazi ya uwekezaji kwenye ardhi na nyumba ikiwemo mikopo ya ukarabati wa nyumba, mikopo ya kuendeleza nyumba, mikopo ya kupamba nyumba, mikopo ya bustani ya maua kwenye nyumba na kadhalika.
Muhimu; Jiunge na kundi maalum la mafunzo ya uwekezaji kwenye ardhi na nyumba. Nitumie ujumbe WhatsApp usemao " KUNDI LA MAFUNZO".
Mwandishi,
Aliko Musa
WhatsApp; +255 752 413 711
Bofya Hapa Kupata VITABU
www.uwekezajimajengo.wordpress.com/huduma
JKUPATA MASOMO KWA E-MAIL JIUNGE HAPA BURE
www.uwekezajimajengo.substack.com
KUJIUNGA NA KUNDI YA TELEGRAM
https://t.me/joinchat/Ydwj2U9-NKtmMGY0
Karibu sana