Jinsi Ya Kuandika Mpango Mkakati Wa Udalali Wa Viwanja Na Nyumba
Kwenye mazingira yetu ya Tanzania dalali ni moja ya mbobezi kwenye viwanja na majengo ambaye hamiiniki kabisa. Kila mmoja ana uzoefu wake binafsi unaochangia kutowaamini madalali wa viwanja na nyumba.
Kukosa kuaminika kwa asilimia kubwa ya madalali wa viwanja na nyumba ndipo ambapo wengine huona fursa kubwa katika kazi hii ya dalali.
Udalali wa viwanja na nyumba ni kazi halali kama zilivyo kazi zingine. Ubaya wa madalali hauwezi kubadilisha ukweli kuwa udalali ni kazi halali kwa asilimia 100 na unatambulika na kukubalika na serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uchanga wa mifumo ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo ni sababu mojawapo ya kuwepo kwa chanagamoto mbalimbali za madalali wa viwanja na majengo.
Kukosa maarifa sahihi kwa asilimia kubwa ya wawekezaji kwenye ardhi na majengo ni sababu nyingine inayosababisha kuendelea kuwepo kwa chanagamoto zitokanazo na madalali wa ardhi na majengo.
Mbali na kuwepo na changamoto tofauti tofauti za udalali wa viwanja na majengo, inawezekana kabisa kutengeneza kiasi kikubwa cha fedha.
Kwenye ukurasa huu ninakushirikisha namna ya kuandika mpango mkakati wa udalali wa viwanja na majengo. Mpango mkakati huu utakusaidia kupata mafanikio makubwa kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Tafadhali bobea kwenye huduma za udalali wa viwanja, mashamba na majengo tu. Kufanya huduma za udalali wa kila kitu ni kupoteza muda tu. Utakuwa unatoa huduma za hovyo kwa kufanya udalali wa kila kitu.
Majukumu Ya Dalali Wa Viwanja Na Majengo.
Moja; kutafuta wawekezaji wanunuzi wa viwanja na majengo.
Pili; kutafuta wawekezaji wauzaji wa viwanja na majengo.
Tatu; kusimamia na kushauri mambo yahusuyo uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
Nne; kubobea kwenye mambo mengine yahusuyo uwekezaji kwenye viwanja na majengo ikiwemo kuthamini nyumba, kukagua nyumba na kuandika ripoti za ukaguzi wa nyumba, kuunganisha fursa za mikopo ya majengo na kadhalika.
Vipengele Vya Mpango Mkakati Wa Udalali.
Mpango mkakati unaweza kuwa ni kwa muundo wa kila wiki, mwezi au mwaka. Kwenye ukurasa huu ninakushirikisha mpango mkakati wa mwaka.
Ukihitaji mpango mkakati wa mwezi unabadilisha kichwa cha mwaka na kuwa mwezi. Unaweza kufanya hivyo pia unapotaka kuufanya mpango mkakati wa mwaka kuwa mpango mkakati wa wiki.
(a) Kutengeneza mtandao.
Hapa unaoongeza idadi ya mashabiki wako wa udalali wa viwanja na majengo. Hapa unatakiwa kutenga kwenye vipengele viwili; wanunuzi na wauzaji wa viwanja na majengo.
Hapa unatakiwa kuandika vipengele vifuatavyo;-
✓ Wauzaji uliowafikia.
✓ Asilimia ya wauzaji ambao wametoa ahadi.
✓ Wauzaji waliotimiza ahadi.
✓ Wanunuzi uliowafikia.
✓ Asilimia ya wanunuzi waliotoa ahadi.
✓ Wanunuzi waliotimiza ahadi zao.
(b) Mtangazo ya kamisheni.
Je umepokea matangazo mangapi ya viwanja na majengo?. Uhitaji kuwahudumia watu wengi zaidi ili uweze kutengeneza kiasi kikubwa cha fedha.
Hapa ni pale ambapo una jukwaa la kuwatangazia wateja wako huduma za udalali wa ardhi na majengo.
Hapa unatakiwa kuwa na vipengele vinne (04) kama ifuatavyo;-
✓ Asilimia ya wauzaji waliotimiza ahadi zao.
✓ Idadi ya wauzaji waliolipia matangazo kwako.
✓ Asilimia ya wanunuzi waliotimiza ahadi zao.
✓ Wanunuzi waliolipia huduma zako za matangazo.
(c) Mikataba Iliyoandikwa.
Hapa unatakiwa kugawa mkakati wako kwenye vipengele vifuatavyo;-
✓ Asilimia ya wauzaji walioingia makubaliano na wewe.
✓ Wauzaji waliosaini mkataba tayari.
✓ Asilimia ya wanunuzi walioingia makubiliano na wewe.
✓ Wanunuzi waliosaini mikataba tayari.
✓ Jumla ya mikataba ya wauzaji.
✓ Jumla ya mikataba ya wanunuzi.
✓ Jumla ya mapato ghafi (Gross income) kutoka kwa wauzaji.
✓ Jumla ya mapato ghafi kutoka kwa wanunuzi.
(d) Mikataba Iliyokamilika.
Hii ni mikataba ambayo mauzo na manunuzi yake yamekamilika kwa asilimia 100. Hivyo hutahitajika tena kutoa huduma za udalali wa viwanja na nyumba.
Hapa hujumuisha vipengele vifuatavyo vya mpango mkakati huu;-
✓ Jumla ya mikataba ya wauzaji iliyokamilika
✓ Jumla ya mikataba ya wanunuzi iliyokamilika.
✓ Jumla ya mapato ghafi kutoka kwenye mikataba ya wauzaji Iliyokamilika.
✓ Jumla ya mapato ghafi kutoka kwenye mikataba ya wanunuzi Iliyokamilika.
(e) Fedha.
Hapa unatakiwa kuwa na vipengele vifuatavyo;-
✓ Jumla ya mapato ghafi yote.
✓ Gharama za mauzo.
✓ Gharama za uendeshaji.
✓ Mapato halisi (net incomes).
Hivi ndivyo vipengele vya muhimu sana kwenye mpango mkakati wako wa utoaji wa huduma za udalali wa viwanja na majengo.
Unaweza kuboresha huduma zako kwa viwango vya juu sana endapo unatabia ya kufanya kazi kwa kufuata mpango mkakati wa aina hii.
Kama ulikuwa unatoa huduma za udalali wa viwanja na majengo kwa mazoea, tafadhali badilika.
Utaona matokeo makubwa ya kuongezeka kwa mapato yako halisi yatokanayo na huduma za udalali wa viwanja na majengo.
Mbali na kuwa na mpango mkakati mzuri, unahitaji kuwa na tabia njema kama vile lugha nzuri, uaminifu, bidii katika kazi, kutunza muda na kadhalika.
Unaweza kufungua jukwaa la kutoa ushauri mambo mbalimbali yahusuyo ardhi na majengo kwa upande wa udalali. Hapa utashauri wawekezaji mambo yote uliyopata na kujifunza wakati wa utoaji wa huduma zako za udalali wa viwanja na majengo.
Jukwaa linaweza kuwa ni ukarasa wa facebook, blogu, ukurasa wa instagram, na akaunti ya YouTube.
Kurasa za facebook na instagram zina wafuasi wengi sana. Hivyo utawafikia wanunuzi na wauzaji wengi wakati unatangaza viwanja au nyumba za wateja wako.
Karibu ujiunge na huduma zangu ili nikusimamie kwenye huduma zako za udalali wa viwanja na majengo. Hakika huduma zako zitaboreshwa sana na kipato chako kitaongezeka. Karibu.
Muhimu; Nitumie ujumbe " Kundi La UWEKEZAJI MAJENGO" ili kupata utaratibu wa kujiunga na kundi maalumu la mafunzo ya uwekezaji katika viwanja na nyumba.
Mwandishi,
Aliko Musa
WhatsApp; +255 752 413 711
Huduma zote ninazotoa hizi hapa chini, Bofya na usome...
www.uwekezajimajengo.wordpress.com/huduma
KUJIUNGA NA KUNDI YA TELEGRAM
https://t.me/joinchat/Ydwj2U9-NKtmMGY0
Karibu sana