Jinsi Mwajiriwa Anavyoweza Kujenga Utajiri Kwa Kumiliki Nyumba Za Kupangisha Zenye Kipato Kikubwa
Tunatafuta usalama na uhuru.
Usalama na uhuru ndiyo huendesha maisha ya watu wote duniani. Kwenye ukurasa huu nina kuonyesha makundi makuu mawili (2).
Kundi la kwanza ni lile linalotafuta usalama wa maisha yao ya kifedha. Kundi la pili ni lile ambalo wanatafuta uhuru wao wa maisha yote.
Usalama.
Your security.
Uhuru.
Freedom.
Waajiriwa hutafuta usalama. Usalama wa kupata chakula, mavazi, matibabu na kadhalika.
Wawekezaji na wafanyabishara hutafuta uhuru wa maisha ya familia zao, ndugu zao, furaha yao na kadhalika.
Mara zote, waajiriwa hukosa usalama wa kila kitu kwenye maisha yao kwa sababu wameajiriwa. Hukosa muda wa kujenga mahusiano bora na wenza wao.
Waajiriwa hukosa uhuru wa kufanya maamuzi kuhusu yale wanayoyataka kwenye maisha yao.
Waajiriwa hukosa uhuru wa kuabudu kulingana na imani zao. Waajiriwa hukosa muda wa kuwalea watoto katika malezi bora na yenye tija.
Kuna kundi dogo mno ambao huajiriwa na kutafuta uhuru kwa kutumia muda wao wa ziada.
Waajiriwa hawa hujinyima kila kitu ili waanze kuwekeza kwenye ardhi na majengo kwa ajili ya kuongeza kipato. Hatimaye wapate uhuru wa kila kitu kwenye maisha yao.
Kundi hili la waajiriwa ni dogo sana na wakati mwingine huonekana kuwa wanajitesa pasipokuwa na sababu za msingi.
Sababu Za Mwajiriwa Kuanza Kuwekeza Kwenye Majengo Ya Kupangisha.
MOJA.
Majengo ya kupangisha huhitaji muda mchache wa kusimamia. Unaweza kutumia siku za sikukuu au muda wa siku za wikiendi kufanya uwekezaji wako.
Kwa kazi za jeshi na kazi nyingine ambazo muda wa kutafuta nyumba na kusimamia ni mdogo sana. Mkewako au mtu yeyote wa karibu anaweza kusimamia.
Utakachokuwa unafanya ni kujenga mfumo mzuri wa kutunza nakala muhimu za uwekezaji wako na mfumo bora wa kutunza fedha zako.
PILI.
Ajira Yako Ni Chanzo Kikuu Cha Mtaji Fedha.
Ni rahisi kutumia sehemu ya mshahara wako kuanza kuwekeza kwenye ardhi na majengo ya kupangisha
Na unaweza kutengeneza kipato endelevu ndani ya mwezi mmoja tu. Unachohitaji ni kuwa na maarifa sahihi na mshauri mbobezi kwenye majengo ya kupangisha.
TATU.
Ubora Wa Kutoa Huduma Kwenye Eneo La Kazi Utaongeza.
Hii ni kwa sababu mawazo ya kukopa huku na kule ukiwa unasubiri mshahara yanakuwa yamekoma. Kwa jinsi hii itakuwa rahisi kuwa na furaha katika eneo lako la kazi.
Itafikia mwaka ambao kipato cha majengo yako ni mara tano, au kumi na hata mara mia ya kiwango cha mshahara wako.
Jambo ambalo utaweza kuondoa kabisa hofu ya kufukuzwa kazi au huduma unayotoa. Kama ni kazi ya uchungaji ambayo kwa wengi ni wito huwezi kuacha.
Utaendelea kuwahubiria watu wamheshimu Mungu wao pasipo kuathiri huduma zako za kichungaji. Pia, itakuwa ni nafasi kubwa kwako ya kuwasaida wasiojiweza.
Sina maana unatakiwa kuacha kazi. Nina maana ukiwa umeajiriwa una vyote viwili mkononi; UHURU NA USALAMA.
Kwa mfanyabiashara ana uhuru pekee yake hata kama ataanza kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha.
Leo ninakushirikisha wewe mwajiriwa. Ninakusihi uungane nami na nitakuonyesha njia za kuanza kuwekeza ukiwa umeajiriwa bila kuacha ajira yako.
Usiache ajira ukiwa na lengo la kukimbia changamoto za kuajiriwa. Acha ajira ukiwa umekosa muda wa kusimamia nyumba zako za kupangisha zinazoingiza kipato zaidi ya mara tano, mara kumi, mara mia au zaidi ya mshahara wako.
NNE.
Ni Rahisi Sana Kukuza Uwekezaji Kwenye Majengo Ya Kupangisha.
Ni rahisi kukuza uwekezaji wako kwenye majengo ya kupangisha hata kama bado umeajiriwa. Wapo wanaofanya kazi za majengo ya kupangisha kwa saa kumi (10) kwa kila wiki.
Wengine hufanya kazi saa chache zaidi ya hapo. Hii inatokana na urahisi wa kusimamia nyumba za kupangisha ukilinganisha na kununua na kuuza nyumba au viwanja.
Nyumba moja inayoingiza kipato chanya inaweza kutumika kununua nyumba nyingine ya kipato chanya. Ndani ya miaka mitano unaweza kuwa na nyumba kumi (10) au zaidi za kipato chanya.
Hii inawezekana ukiwa umeajiriwa hata bila kuathiri majukumu yako ya kazi. Inawezekana kabisa.
Imewezekana kwa wengi.
Wengi wameweza.
Fanya wewe sasa.
Ukiwa umeajiriwa kuanza kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha ni rahisi. Ni rahisi hasa kama huna mikopo mibaya.
Kwa kuwa waajiriwa wengi wapo kwenye bahari ya kudaiwa, inakuwa vigumu kwao kuanza kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha.
Makosa Ya Kuepuka Unapowekeza Ukiwa Umeajiriwa.
(i) Usiwekeze Pekee Yako.
Nina maana usifanye shughuli za uwekezaji bila kuwa na timu ya kukusaidia. Huwezi kutafuta nyumba mwenyewe, huwezi kutafuta wapangaji mwenyewe, huwezi kusimamia wapangaji mwenyewe.
Huwezi kupata muda wa kujifunza mambo mazuri ya uwekezaji kwenye majengo ya kupangisha. Huwezi kujishauri kuhusu sheria za umiliki wa ardhi, sheria za wapangaji na mwenye nyumba na kadhalika.
Kila mwekezaji anahitaji kuwa na timu ya kumuwezesha kujenga utajiri kupitia ardhi na majengo.
Lakini kwa mwajiriwa ni lazima uwe na timu ya kukusaidia kujenga utajiri kupitia majengo ya kupangisha. Bila kufuata hili, umeshindwa tayari kwenye uwekezaji wako.
(ii) Kutoweka Akiba Kila Mwezi.
Anza Kuweka Akiba Mwezi Ujao.
Hakikisha unaweka akiba. Weka akiba hata kama bado hujajifunza vizuri kuhusu majengo ya kupangisha. Baada ya miezi mitatu hadi sita, utakuwa umejifunza mambo ya msingi ya kuzingatia.
Ukifanya kosa la kuendelea kutoweka akiba, utachelewa sana kumiliki nyumba za kupangisha. Inawezekana usimiliki kabisa mpaka unazeeka.
(iii) Kutojifunza Kila Wiki.
Kwa mwajiriwa, unatakiwa kutumia siku za wikiendi kujifunza na kupitia ripoti mbalimbali za uwekezaji wa majengo ya kupangisha.
Kuacha kujifunza na kusubiri miaka ijayo utakapoanza kuwekeza ndiyo itakayo kuwa moja ya sababu za kushindwa kwako.
Unaweza kutenga hata nusu saa kila siku baada ya kutoka kazini kujifunza kuhusu majengo ya kupangisha.
Kwa kufanya hivi, itakuwa vigumu kufanya makosa yanayotokana na ujinga wa mwekezaji.
Hatimaye mwajiriwa atakuwa salama kwa sababu anaingiziwa mshahara kila mwezi.
Vilevile mwajiriwa huyo atakuwa huru kwa sababu ya kiasi kikubwa cha kipato endelevu kutoka kwenye majengo yake ya kupangisha.
Muhimu; Lipia elfu arobaini (Tshs.40,000/=) ili ujifunze mambo mazuri ya uwekezaji kwenye viwanja na majengo. Kwa malipo haya utajifunza miezi sita (6) mfululizo.
Mwandishi,
Aliko Musa
WhatsApp; +255 752 413 711
Huduma zote ninazotoa hizi hapa chini, Bofya na usome...
www.uwekezajimajengo.wordpress.com/huduma
KUJIUNGA NA KUNDI YA TELEGRAM
https://t.me/joinchat/Ydwj2U9-NKtmMGY0
Bofya hapa, kisha andika barua pepe (email) yako ili uendelee kupata masomo mazuri ya ardhi na majengo.