Hatua Nane (8) Za Kujenga Mfumo Mzuri Wa Kusimamia Nyumba Za Kupangisha
Usimamizi bora wa nyumba za kupangisha kuongeza kiasi cha kodi ya kila mwezi.
Faida za kusimamia wewe mwenyewe nyumba yako ya kupangisha (self-management) ni kama ifuatavyo;-
✓ Kutunza fedha ambayo ulitakiwa umlipe msimamizi.
✓ Kupata wapangaji mapema zaidi kwa kuwa unafahamu uchungu wa nyumba yako.
✓ Kupata uzoefu wa usimamizi wa nyumba.
✓ Kupata taarifa muhimu za usimamizi wa nyumba kama vile kuandaa mikataba mizuri ya upangishaji, hali ya masoko tofauti tofauti na kutathimini kiasi sahihi cha kodi.
Hatua Nane (8) Za Kusimamia Nyumba Za Kupangisha Kwa Mafanikio Makubwa.
MOSI.
Andaa Mkataba Wa Upangishaji.
Hakikisha unaanda mkataba wa upangishaji ambao unaendana na wapangaji watarajiwa wa nyumba yako.
Malengo makuu mawili (2) ya mkataba wa upangishaji ni kama ifuatavyo;-
✓ Inakupa ulinzi wewe na uwekezaji wako dhidi ya changamoto tofauti tofauti.
✓ Husaidia kuwashinda washindani wako kwa kuandaa mikataba ya manufaa kwako na kwa wapangaji wako.
PILI.
Andaa Mazingira Mazuri Kwa Wapangaji.
Hakikisha wapangaji wanajisikia vizuri sana wakati wa kuhamia kwenye nyumba yako ya kupangisha.
Hakikisha nyumba ipo kwenye hali ya usafi nje na ndani ya nyumba. Hakikisha vifaa vyote vya ndani na nje ya nyumba zinafanya kazi vizuri.
Soketi za umeme, hita ya maji, kiyoyozi na kadhalika vyote viwe kwenye hali nzuri ya ufanyaji kazi.
Kama nyumba ina samani (furnitures), hakikisha samani zote zipo safi na hazijaharibiwa.
Muonyeshe mpangaji wako kikata umeme (circuit breaker boxes), swichi za balbu na kadhalika.
Hakikisha unatoa maelekezo ya jinsi ya kutumia vifaa vyote vilivyomo ndani ya nyumba hasa vifaa vya umeme.
Andaa ramani ya kuonyesha huduma zinazozunguka nyumba atakayokuwa anaishi. Huduma za maduka, shule, chuo, bohari, fremu za biashara, huduma za ushauri na migahawa.
Orodha ya huduma hizi iwe na mawasiliano hasa namba za simu zinazopatikana na sio namba ambazo hazitumiki.
Haya ni baadhi ya mambo ambayo yatamfanya mpangaji wako kuwa na furaha kipindi cha uhamiaji kwenye nyumba yako.
Hakikisha mpangaji anasaini ripoti ya ukaguzi wakati wa kuingia kwenye nyumba yako. Hii itakuwa ni ushuhuda wakati wa kutoka kwenye nyumba yako kuwa hajaharibu au kuchukua vifaa vyako.
TATU.
Mjali Mpangaji Wako.
Mfanye mpangaji wako kuwa mwenye furaha. Mfanye mwenye furaha mpaka tukio ambalo lipo nje ya uwezo wako litokee kuharibu furaha yake.
Wape taarifa zote wapangaji wako zile wanazotakiwa kuwa nazo. Wape taarifa hizo kwa muda sahihi na kwa njia sahihi.
Panga ukarabati kinga (preventive maintenance). Huu ni ukarabati utaokusaidia kupoteza fedha nyingi wakati wa ukarabati wa dharura.
Tegemea yasiyo tegemewa. Kwenye usimamizi wa nyumba za kupangisha huweza kutokea matukio yasiyo tegemewa. Jiandae kiakili kwa hili.
NNE.
Pandisha Kiasi Cha Kodi.
Pandisha kiasi cha kodi ya nyumba kipindi ambacho hali ya soko mahalia liko vizuri.
Hii itakusaidia kuongeza kiasi cha kipato endelevu cha kila mwezi. Wawekezaji wengi husahau kazi ya kupandisha kodi ya nyumba kwa wakati sahihi. Hutakiwi kufanya kosa la namna hii.
TANO.
Karabati Nyumba Iwe Kwenye Mvuto.
Usikubali nyumba yako ishuke viwango vya mvuto kutoka kwa wapangaji. Wapangaji wasiichoke nyumba yako.
Kwa kuongezea aina za ukarabati kutoka kwa ukarabati kinga, tunapata aina nyingine za ukarabati. Aina hizo ni kama ifuatavyo;-
✓ Ukarabati wa kila siku (custodial maintenance). Kusafisha bustani, kuokota makopo na uchafu mwingine kuzunguka nyumba, kusafisha nje ya madirisha, na kuifanya nyumba yako safi na yenye mvuto.
Jambo hili ni muhimu sana kwenye majengo ya apatimenti kubwa, hoteli, resoti, hosteli na ini.
✓ Ukarabati wa urembo (cosmetic mainataince). Kuboresha maeneo ya kolido, kuhakikisha kapeti zipo kwenye hali ya kuvutia, kuondoa weusi kwenye balbu na kurekebisha rangi ya ukuta na bati.
✓ Ukarabati wa kiulinzi na kiusalama (safety and security maintenance). Ngazi za nyumba, balbu za mwanga getini, makufuri, milango na madirisha.
Vyote hivi viwe katika hali nzuri ifanyayo kazi. Vitu hivi vinatakiwa viwe imara na salama. Hakikisha unamsisitiza mpangaji kutoa taarifa mapema shida yoyote kubwa inapotokea.
SITA.
Muondoe Mpangaji Kwa Amani.
Kamwe usitumie matusi na nguvu na ugomvi kumuondoa mpangaji. Mpangaji ikitokea ameamua kudai haki zake mahakamani, utapata tabu sana.
Uwekezaji wako utakuwa umeuweka matatizoni. Unaweza kupewa faini au kupewa adhabu utakayostahili kulingana na kosa au makosa yako.
Pia, itakufanya wapangaji watarajiwa waogope sana kuja kupanga kwako. Mpangaji mkishindwana muondoe kwa amani.
SABA.
Tafuta Njia Za Kuongeza Kipato Endelevu Cha Kila Mwezi.
Kuna njia kuu (2) za kuongeza kiasi cha kipato endelevu cha kila mwezi. Nazo ni;-
✓ Kuwekeza kwako mwenyewe. Hakikisha wewe mwenyewe (kama msimamizi) unahudhuria semina za upangishaji wa nyumba, unasoma vitabu vya upangishaji wa nyumba, na unakuwa na menta au kocha wa nyumba za kupangisha.
✓ Tumia fedha kwenye maeneo ambayo huongeza thamani kubwa ya kufikirika na thamani inayodumu kwa muda mrefu.
NANE.
Jiandae Kwa Chanagamoto Maalumu.
Hakikisha mkataba unaeleza jinsi msimamizi utakavyo shughulikia chanagamoto kubwa na za dharura kwa wapangaji wako.
Chanagamoto za kifo, talaka, ajali, magonjwa, kufukuzwa kazi, kupoteza nafasi ya kazi, kupunguziwa mshahara kazini, kusimamishwa kazi, kufunguliwa kesi za jinai na kufungwa kwa wapangaji au ndugu wa karibu wa wapangaji.
Mambo yote haya hakikisha unajiandaa kushuhulikia. Unaweza kueleza kuwa wapangaji wanatakiwa kuomba au kukopa fedha za jamaa zao wa karibu.
Au kutumia njia yoyote halali ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kulipia kodi ya pango la nyumba. Njia zinaweza kujumuisha kuwashauri wapangaji kuanzisha biashara ya pembeni.
Kwa wapangaji ambao kila njia ya kupata kodi imeshindikana baada ya kupatwa na majanga haya. Unaweza kuwaacha waende bila kukulipa kodi ya pango la nyumba.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Muhimu; Lipia elfu arobaini (Tshs.40,000/=) ili kupata ushauri, semina, darasa la kila jumapili na makala za kila siku za kulipia. Kwa malipo haya utajifunza miezi sita (6) mfululizo.
Mwandishi,
Aliko Musa
WhatsApp; +255 752 413 711
Bofya hapa kujiunga na kundi la Telegramu la ARDHI NA NYUMBA CLUB
https://t.me/joinchat/Ydwj2U9-NKtmMGY0
Bofya hapa kujiunga na kundi la WhatsApp la ARDHI NA NYUMBA CLUB
https://chat.whatsapp.com/FeMEt5K2mYbKNYoPR8tRdX
Bofya hapa, kisha andika barua pepe (email) yako ili uendelee kupata masomo mazuri ya ardhi na majengo.