ARDHI 09:Panda Miti Ya Matunda Ya Kudumu (Maembe, Nazi, Parachichi, Machungwa, Machenza)
Utangulizi
Ikiwa una kipande cha ardhi kuanzia nusu ekari, unaweza kupanda miti ya matunda. Miti hii inaweza kukuletea manufaa makubwa ya kifedha kuliko kukaa na ardhi miaka mingi bila manufaa yoyote.
Kama kweli unahitaji pesa kwa ajili ya kuendesha maisha yako na familia yako, hakikisha unatumia kuingiza pesa.
Fuatana na hadi mwisho wa masomo haya upate maarifa ya kutengeneza pesa katika ardhi na nyumba.
Faida Ya Kutengeneza Pesa Kupitia Njia Hii
Moja, utapata manufaa ya kudumu. Utajipatia fedha kwa ajili kuwekeza katika ardhi na nyumba.
Kwa ndio uwekezaji wa uhakika na wenye hatari ndogo ya kupoteza mtaji fedha wako.
Mbili, kulinda usalama wa umiliki wa ardhi yako. Ardhi ambayo haiendelezwi wala kufanyiwa shughuli yoyote ya kiuchumi na kijamii, umiliki wake upo hatarini.
Hii ni kwa sababu serikali huhimiza watu wake kuendeleza ardhi wanazomiliki kwa niaba ya serikali yenyewe.
Tatu, ardhi yako inaongezeka thamani. Unaweza kuitumia kupata mkopo au kuuza kwa bei ya juu ikiwa na matunda ya kuuza.
Ardhi ambayo haina chochote, huuzwa kwa bei ya chini na uhakika wa kuchukua mikopo unakuwa mdogo sana.
Changamoto Za Kutengeneza Pesa Kupitia Njia Hii
Moja, utahitaji uzoefu na maarifa kuhusu kilimo cha matunda utakayopanda.
Hivyo kukosa uzoefu na maarifa kutapelekea kukosa kipato cha uhakika kutoka katika matunda yako.
Mbili, matunda ya kudumu huleta faida baada ya miaka minne na kuendelea. Hivyo njia hii inahitaji subira sana.
Tatu, soko la matunda haya linaweza kuwa changamoto kubwa katika nchi zetu zinazoendelea isipokuwa nazi ambayo haiharibiki kwa urahisi.
Nne, utahitaji mtaji fedha kwa kipindi chote, kuanzia uaandaji wa shamba hadi uvunaji wa matumizi yenyewe.
Hivyo kama hauna mtaji fedha, uza sehemu fulani na panda matunda. Au tafuta mkulima wa matunda, umpangishie kipande cha ardhi yako.
Ushauri
Njia hii itakupatia kipato cha kudumu na utaweza kuwekeza katika ardhi na nyumba kwa urahisi zaidi.
Baada ya kufanikiwa kuanza kupata fedha, kumbuka kuweka katika ardhi na nyumba.
Ukisahau kuwekeza katika ardhi na nyumba, utakuwa unajiumiza wewe mwenyewe.
Mwandishi,
Aliko Musa.
WhatsApp: +255 752 413 711
Karibu sana.