Aina Ya Nyumba Ya Kupangisha Inayofaa Kwa Wawekezaji Wanaoanza
Changamoto kwa wawekezaji wengi wanaoanza kuwekeza kwenye nyumba za kupangisha ni kama vile;-
✓ Kukosa mtaji wa kutosheleza kumiliki nyumba kubwa za kibiashara za kupangisha (commercial properties).
✓ Kukosa ushauri bora wa uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
✓ Kukosa uzoefu wa jinsi ya kuchagua au kujenga nyumba inayolipa kwa ajili ya kupangisha mpaka kujenga himaya yake ya utajiri.
✓ Kukosa miongozo yenye vigezo bora vya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.
✓ Kukosa maarifa sahihi ya kuchagua aina ya jengo la kupangisha linalofaa kwa kuanzia kuwekeza.
Kwa ujumla, inachukua miaka mingi kurekebisha kosa la kiuwekezaji katika ardhi na majengo. Makosa kama kuchagua kiwanja kisicholipa, nyumba ambayo hailipi, ramani ambayo hailipi, kutumia fedha nyingi kwenye ujenzi kuliko inavyotakiwa, kutumia gharama kubwa za ukarabati kuliko inavyotakiwa ni moja ya makosa ambayo yanaacha maumivu makali kwa miaka bila kupata suluhu sahihi.
Makala hii ni sehemu tu ya wewe kukuandaa uweze kupunguza au kuondoa changamoto za uwekezaji kwenye nyumba za kupangisha kipindi cha mwanzo wa safari yako ya uwekezaji.
Aina Ya Kwanza.
Majengo ya matumizi mseto.
Je nyumba za matumizi mseto (mixed-use properties) hufaa kwa wawekezaji wanaoanza?.
Nyumba za matumizi mseto ni aina ya nyumba ambazo hutumika kwa ajili ya makazi na au biashara. Nyumba hizi hufaa zaidi kwa wawekezaji ambao wanahitaji kutumia baadhi ya vyumba kwa ajili ya kuishi wao wenyewe na vyumba vingine vitumike kupangisha kwa wapangaji bora.
Aina Ya Pili.
Majengo ya biashara.
Je majengo ya biashara yanafaa kuanza kujenga utajiri kwa wawekezaji wanaoanza?.
Majengo ya biashara ni kundi la majengo ambayo hutumika kwa kutoa au kuwezesha biashara za huduma au biashara za bidhaa au vyote viwili kwa wakati mmoja. Majengo ya biashara ni majengo ambayo hayatumiki kwa ajili ya kuishi. Ni majengo yanayotumika kwa ajili ya biashara tu.
Majengo ya biashara yapo katika makundi manne; bohari/Godauni (stoo), fremu za biashara, majengo ya viwanda na majengo ya viwanda.
Lakini majengo ya familia nyingi (multifamily properties) huingia kwenye kundi la majengo ya biashara kwa sababu hutumika au huchukuliwa kibiashara na mmiliki wa jengo husika.
Mfano ni hosteli za wanafunzi hata kama hutumika kwa ajili ya kuishi lakini huingia kwenye majengo ya biashara kwa hutumika kibiashara na mwekezaji husika.
Faida za majengo ya biashara;
✓ Huhitaji kiasi kikubwa sana cha mtaji fedha ukilinganisha na majengo ya familia chache. Lakini huhitaji kiasi kidogo cha mtaji ukilinganisha na majengo ya familia nyingi.
✓ Huingiza kiasi kikubwa cha kodi ya kila mwezi ukilinganisha na bei inayouzwa.
✓ Huhitaji kiasi kidogo cha gharama za ukarabati wa majengo ukilinganisha na majengo ya familia nyingi.
Changamoto za majengo ya biashara.
✓ Huhitaji kiasi kikubwa cha mtaji fedha ukilinganisha na majengo ya familia chache.
✓ Huhitaji uchaguzi mzuri wa eneo la kujenga majengo ya biashara.
Aina Ya Tatu.
Majengo ya familia nyingi (multifamily properties).
Faida zake.
✓ Huingiza kiasi kikubwa cha kipato endelevu kwa kila mwezi ukilinganisha na majengo ya familia chache.
✓ Huhitaji kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya ukarabati kwa sababu ya kuwa na paa moja na mifumo inayofanana.
Hasara zake.
✓ Ni vigumu kusimamia na kupangisha kwa kuwa wapangaji huhamia nyumba zingine ndani ya muda mfupi.
✓ Hatari kubwa za upotevu wa kipato endelevu.
✓ Kupanda na kushuka kwa thamani ya majengo mara kwa mara.
✓ Ni vigumu kuombea mikopo ya majengo.
✓ Ni vigumu kuuza jengo la aina hii kwa kipindi cha kufanya mauzo.
Rafiki yako,
Aliko Musa.
Mbobezi majengo.